KIPIMO CHA VYOMBO VYA HABARI BARANI AFRIKA Tanzania 2019 Muhtasari Mwaka 2015, Tanzania ilifanya uchaguzi mkuu ambao ulimweka madarakani Rais wa sasa Mheshimiwa John Pombe Magufuli. Kwa muda mfupi, Rais Magufuli alikubalika na wengi kutokana na jitihada zake za kupambana na rushwa ambazo zimesababisha maofisa wengi wa serikali kutolewa katika nafasi zao. Utawala huu mpya pia umechukua hatua madhubuti kuongeza nidhamu katika utumishi wa umma. Hata hivyo, mtindo wa utawala wa Rais Magufuli na hasa kuhusu uhuru wa kujieleza na uhuru wa habari umekuwa chanzo cha madhila makubwa. Kwa kiasi kikubwa, amejiimarisha kiutawala na kuhodhi maamuzi ili kujijengea umaarufu; vyama vya siasa vya upinzani vimeminywa, wakosoaji wa serikali wamekuwa wakikamatwa, na haki ya msingi ya uhuru wa kujieleza imeathirika vibaya. Mambo haya yanayoogofya ni sehemu tu ya mabadiliko katika nyanja nyingi nchini Tanzania katika kipindi cha miaka minne iliyopita. Ingawa Tanzania ina katiba ambayo imeeleza haki za msingi za kiraia na za kisiasa, ikiwa ni pamoja na uhuru wa kukusanyika na uhuru wa kujieleza, haki hizi zimeminywa. Katika kipindi cha miaka mitatu tangu mwaka 2015, sheria kadha wa kadha za vyombo vya habari zilipitishwa, ikiwemo Sheria ya Vyombo vya Habari ya mwaka 2016, ambayo ina mianya na madhaifu mengi yanayominya uhuru wa kujieleza. Sheria hii inaipa serikali mamlaka makubwa juu ya maudhui ya habari na utoaji leseni kwa vyombo vya habari na waandishi wa habari. Sheria hii pia inaweka adhabu kali, ikiwemo kifungo gerezani, endapo chombo cha habari kitachapisha habari za kuikashfu serikali, uchochezi, au maudhui mengine yasiyozingatia sheria. Wakati wanajopo wakiendelea na mjadala, mabadiliko ya hivi karibuni ya Sheria ya Takwimu ya Mwaka 2015 yanamtaka mtu yeyote au taasisi kupata idhini ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kabla ya kutoa takwimu kwa matumizi ya umma. Sheria hii ilibadilishwa katika kipindi cha nusu mwaka wa 2019 na kwa hivyo haizuii tena kuchapisha taarifa ya kitakwimu bila kupata ishini ya ya serikali, lakini bado takwimu rasmi zimeendelea kuhitaji kibali cha NBS. Mnamo mwezi Machi, kabla ya mabadiliko ya hivi karibuni, sheria hii ilitumika kufungia gazeti linalomilikiwa na mtu binafsi la The Citizen kwa madai kwamba lilichapisha taarifa za uongo, zenye kupotosha na za kichochezi. Gazeti hilo lilichapisha habari kuhusu kushuka thamani kwa shilingi ya kitanzania (TZS) dhidi ya Dola ya Kimarekani (US$). Mnamo mwezi Machi 2018, serikali iliweka Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (mtandaoni), ambao uliwataka wamiliki wa blogu na waendeshaji wa 6 KIPIMO CHA VYOMBO VYA HABARI BARANI AFRIKA TANZANIA 2019