mijadala kupitia majukwaa ya mtandaoni kulipa zaidi ya US$ 900 kwa mwaka
kama ada ya kujiandikisha. Kanuni hizi zilitolewa chini ya Kifungu cha 103(1)
cha Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta ya Mwaka 2010. Kanuni
hizo pia zinatoa mamlaka kwa Mamlaka ya Usimamizi wa Mawasiliano Tanzania,
ambayo ndio msimamizi wa mawasiliano Tanzania, kuondoa habari mtandaoni.
Mamlaka haya hayana kinga yoyote dhidi ya matumizi yasiyo ya haki. Mathalan,
ada zinazowekwa na kanuni hizo zilisababisha kufungwa kwa muda kwa Jamii
Forum, ambao ni mtandao maarufu na jukwaa la habari, mwaka 2018. Kanuni
hizi vilevile zinawawajibisha watumiaji wa mitandao ya kijamii kwa mahudhui
ambayo ‘si ya kistaarabu, yenye kashfa, au yanayoweza kusababisha chuki kwa
jamii,’ pamoja na vifungu vingine vyenye utata.
Watumiaji wa mitandao ya kijamii hali kadhalika wako kwenye hatari ya
kushtakiwa chini ya Sheria ya Makosa ya Kimtandao ya mwaka 2015, ambayo
inazuia, pamoja na mambo mengine, kumtukana Rais mtandaoni. Serikali
pia imetishia kuwashtaki watumiaji wa mitandao ya kijamii watakaoshukiwa
kueneza ushoga kwa kupitia mitandao ya kijamii; kwa mujibu wa sheria iliyopo
sasa, ushoga ni kinyume cha sheria za nchi. Makundi na watetezi wanaotetea
haki za wasagaji, mashoga, na watu wenye tabia za jinsia mbili (LGBTQIA+) pia
wamekuwa wakinyanyaswa. Mwaka 2018, serikali ilitangaza kuunda kikosi
maalum cha doria kwa lengo la ‘kuwasaka’ watu wanaojihusisha na ushoga.
Uhuru wa kukusanyika pia umeminywa na kumekuwepo na zuio la mikutano
ya kisiasa na maandamano ya umma tangu mwaka 2016, pamoja na kwamba
Katiba inatoa haki hii. Mikusanyiko yote sharti ipate kibali cha polisi na
maandamano ya kisiasa yamezuiliwa kwa nguvu zote kwa nyakati tofauti. Kitu
pekee kinachoruhusiwa ni mikutano ya kisiasa inayofanywa na wabunge kwenye
majimbo yao ya uchaguzi; ambapo kwa kiasi kikubwa kinawapa faida wabunge
wanaotokana na chama tawala, Chama cha Mapinduzi -kwa kuwa kina wabunge
wengi wanaotokana na majimbo ya uchaguzi. Serikali imeanza kutumia vifungu
vya zamani vya sheria na sheria ya kikoloni ya watu wasiokubalika ambayo
inapiga marufuku uzururaji, ili kuzuia vijana kukaa vijiweni au kukusanyika.
Pamoja na kwamba jitihada zimefanyika kuboresha upatikanaji wa habari,
uhalisia wa haki hii umeendelea kuwa changamoto kubwa. Baada ya miaka
mingi ya kupigania haki za vyombo vya habari na haki za binadamu, hatimaye
Tanzania ilipitisha Sheria ya Upatikanaji wa Habari ya mwaka 2018. Pamoja na
vipengele vyenye matumaini vilivyomo kwenye sheria hiyo, kupata habari bado
halijawa jambo rahisi.
Ingawa Tanzania ina wigo mpana wa vyombo vya habari, kwa njia ya maandishi,
vituo vya luninga (TV) na redio, mtandao na blogu, mazingira kandamizi ya
kisheria na udhibiti yanaathiri matumizi na uendeshaji wa majukwaa haya ya
habari. Aidha, mambo mengine yasiyo ya kisheria yanazuia upatikanaji wa
vyanzo vya habari. Bei ya magazeti na bando kwa mfano, vinaathiri upatikanaji
wa magazeti na habari za mitandaoni vijijini na kwa watu wasio na uwezo.
Kupata matangazo ya kidijitali sasa kunazilazimu familia kununua luninga ya
kisasa zaidi au kununua king’amuzi.

7

KIPIMO CHA VYOMBO VYA HABARI BARANI AFRIKA TANZANIA 2019

Select target paragraph3