ENEO LA 4

inajihusisha na ukuzaji wa vyombo vya habari Tanzania. Wanajopo walisema
kwamba mafunzo yanayofadhiliwa na wahisani yana chanagoto zake kwa kuwa
mara nyingi huwa na wigo mdogo na huwalenga waandishi wale wale.
Mafunzo ya ndani na uwezeshaji pia yanapatikana lakini mara nyingi hayaratibiwi
vizuri.

Alama:
Alama za mshiriki mmoja mmoja:
1

Nchi inakidhi kiashiria

2

Nchi inakidhi vipengele vichache tu vya kiashiria

3

Nchi inakidhi vipengele kadhaa vya kiashiria

4

Nchi inakidhi vipengele vingi vya kiashiria

5

Nchi inakidhi vipengele vyote vya kiashiria

Wastani wa alama:
Alama ya miaka iliyopita:

✓

✓

✓

✓✓

✓

✓

✓✓

✓

✓
✓

3.6
2006: 3.2; 2008: 2.3; 2010: 3.3; 2012: 3.7; 2015: 3.9

4.8 Fursa sawa bila kujali asili au ukabila, tabaka,
jinsia, dini na umri unakuzwa kwenye vyombo vya
habari
Vyombo vya habari Tanzania vinaakisi mchanganyiko na mgawanyiko wa jamii
kwa upana wake. Kwa mujibu wa wanajopo, sekta ya habari ina unyanyasaji
wa kingono na ubaguzi wa kijinsia usio wazi. Pamoja na hatua nzuri katika
kukuza usawa wa kijinsia, wanawake wangali wanawakilisha asilimia kiduchu ya
uongozi wa juu kwenye vyombo vya habari vya umma na vile vya binafsi. Katika
sekta nzima, ni wamiliki wawili tu wa vyombo vya habari na wasimamizi wawili
ambao ni wanawake, isipokuwa kwa redio za kijamii ambapo wamiliki watano
kati ya 35 ni wanawake.
Wanajopo walieleza kwamba unyanyasaji wa kingono ni tatizo kubwa kwenye
vyombo vya habari vya Tanzania:
Kumekuwepo na malalamiko lukuki ya ‘rushwa ya ngono.’ Wahariri wa
kiume mara nyingi huomba rushwa ya ngono kutoka kwa waandishi wa
habari wanawake ili tu taarifa zao za habari zipate kuandikwa. Wakati
mwingine hupanga safari na waandishi wa habari wanawake kwa
matumaini ya kufanya nao ngono. Wahanga wa tabia hii ni pamoja na
wanafunzi waliopo kwenye mafunzo kwa vitendo.
Sheria za Tanzania huchukulia ngono iliofanyika kwa sababu ya madaraka ya
mtu kama ubakaji. Mtuhumiwa akikutwa na hatia, anaweza kufungwa hadi
miaka 30 jela. Lakini hii haijaweza kuzuia tabia hii.
Aidha, wanajopo walisema kwamba ubaguzi wa umri ulikuwa unashika kasi.
Kwa sasa kuna upendeleo wa waandishi wa habari vijana zaidi kwenye vyumba

54

KIPIMO CHA VYOMBO VYA HABARI BARANI AFRIKA TANZANIA 2019

Select target paragraph3