ENEO LA 4

vya habari. Katika matukio machache, waombaji kazi wameambiwa kwenye
mahojiano kwamba walikuwa na umri mkubwa sana kwa kazi hiyo. Moja ya
sababu ni mabadiliko ya mandhari ya vyombo vya habari ambayo yamesababisha
mahitaji wa waandishi wa habari wenye ujuzi wa teknolojia ya kisasa. Hata hivyo,
wanajopo walisema bado kulikuwa na fursa kwa ‘walinzi wazee’ ambao ‘mara
zote wanapatia mambo’.
Ubaguzi unaohusisha imani na ukabila unaonekana zaidi kwenye vituo vya redio
za kidini, ambazo huajiri waumini wao. Wanajopo walisema kwamba hakukuwa
na wanawake wenye hijabu kwenye vituo vya luninga na wanawake ambao
wamekuwa wakiomba kuvaa hijabu wamelazimika kuhamia kwenye vituo vya
redio. ‘Hakuna taswira halisi ya Tanzania kwenye vyombo vya habari.’
Tanzania haitambui haki ya mahusiano na uhuru wa kutobaguliwa kwa sababu
ya tabia za kimahusiano. Kimsingi, mahusiano ya jinsia moja ni kinyume na
sheria. Wapenzi wa jinsia moja na LGBTQIA+ nchini kwa ujumla mara nyingi
wamekuwa wakibughudhiwa, na kukamatwa. Wanajopo walisema kwamba
kulikuwa na mashoga wanaojulikana kabisa kwenye vyombo vya habari.

Alama:
Alama za mshiriki mmoja mmoja:

55

1

Nchi inakidhi kiashiria

2

Nchi inakidhi vipengele vichache tu vya kiashiria

3

Nchi inakidhi vipengele kadhaa vya kiashiria

4

Nchi inakidhi vipengele vingi vya kiashiria

5

Nchi inakidhi vipengele vyote vya kiashiria

✓✓✓

✓

✓

✓

✓

✓✓

✓✓✓

Wastani wa alama:
Alama ya miaka iliyopita:

2.7
2006: n/a; 2008: n/a; 2010: 3.5; 2012: 4; 2015: 3.5

Jumla ya alama kwenye sekta 4:

2.7

KIPIMO CHA VYOMBO VYA HABARI BARANI AFRIKA TANZANIA 2019

Select target paragraph3