ENEO LA 4 4.6 Waandishi na wahariri wote hawajichuji Kwa mujibu wa wanajopo, mtindo wa makala na taarifa ya habari umebadilika miaka mingi kadri waandishi wa habari wanavyotambua uwezekano wa kisasi kutokana na kazi zao. Baada ya kufungiwa mara mbili, wanajopo walisema kwamba waliona mabadiliko ya mtindo wa kampuni ya Mwananchi Communications, ambayo huchapisha gazeti la The Citizen na gazeti dada linalotumia lugha ya Kiswahili la Mwananchi, ambalo linasifika kwa kuandika taarifa makini. Kujichuja kumekithiri. ‘Kuna habari ambazo sitazisogelea kwa namna yoyote ile,’ alisema mwandishi mmoja wa habari kwenye jopo. ‘Baadhi ya watu wametoweka.’ Alama: Alama za mshiriki mmoja mmoja: 1 Nchi inakidhi kiashiria 2 Nchi inakidhi vipengele vichache tu vya kiashiria 3 Nchi inakidhi vipengele kadhaa vya kiashiria 4 Nchi inakidhi vipengele vingi vya kiashiria 5 Nchi inakidhi vipengele vyote vya kiashiria Wastani wa alama: Alama ya miaka iliyopita: ✓ ✓ ✓ ✓ ✓ ✓ ✓✓ ✓ ✓✓ ✓ 1.8 2006: 2.1; 2008: 2; 2010: 1.5; 2012: 1.8; 2015: 2.3 4.7 Waandishi wa habari wana vyuo vinavyotoa mafunzo rasmi pamoja na fursa ya kuinua viwango vyao Kuna fursa nyingi za mafunzo ya uandishi wa habari Tanzania. Baadhi ya vyuo vikuu vinavyotoa mafunzo ya uandishi wa habari ni pamoja na : Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine Tanzania, Chuo Kikuu cha Tumaini (Dar es Salaam na Iringa), Chuo Kikuu cha Kiislam Morogoro na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania. Mbali na vyuo vikuu, idadi kubwa ya vyuo vinatoa mafunzo ya uandishi wa habari kwa ngazi ya Stashahada na cheti. Hata hivyo, wanajopo walisema kwamba ubora wa mafunzo wanayopata wanafunzi unahitaji kuboreshwa. Ilielezwa kwamba wahadhiri wengi wa vyuo vikuu hawajawahi kufanya kazi ya uandishi wa habari na hivyo hawana uzoefu katika kuandika habari na kutafuta habari. Fursa nyingine zinapatikana nje ya mfumo wa elimu. Daily News, ambalo ni gazeti linalomilikiwa na serikali, mara nyingi huwapeleka waandishi wa habari nchini China, shukrani kwa ubia na serikali ya China. Mashirika kama vile UNESCO yamekuwa yakijihusisha na mafunzo na kuwezesha redio za kijamii na yamejenga ushirikiano na na vyuo vya uandishi wa habari kutengeneza mfumo wa kujifunza kielektroniki. Washiriki wengine wakuu ni pamoja na BBC Media Action, ambayo 53 KIPIMO CHA VYOMBO VYA HABARI BARANI AFRIKA TANZANIA 2019