ENEO LA 4 4.5 Waandishi wa Habari na vyombo vya habari wana uadilifu na si wala rushwa Uhandishi wa habari wa bahasha ya kahawia, mtindo ambapo waandishi wa habari wanapewa fedha taslimu na vitu vingine vya mkononi ili waipambe taarifa, umeenea sana Tanzania. Kutokana na malipo kiduchu na mazingira mabaya ya utendaji kazi, washiriki walisema kwamba waandishi wa habari walikuwa kwenye hatari ya kupokea rushwa na mara nyingi walipata hisani ya vyanzo vya habari na wenyeji wa matukio. Tabia hii imekithiri wakati wa chaguzi ambapo viongozi wa kisiasa wanadaiwa kuwahonga waandishi wa habari ili kutangaza kampeni zao. Wanajopo walielezea aina ndogondogo za rushwa kama vile kukubali kupewa usafiri, kulipiwa hoteli na zawadi nyingine zisizohusisha fedha na kubadilishana na habari. Maslahi mahsusi ya mmiliki wa chombo cha habari pia yanaathiri jinsi ya kutangaza habari. Wanajopo walisema kwamba wafanyabiashara fulani wasingeweza kuandikwa vibaya kwenye baadhi ya vyombo vya habari kutokana na ukaribu wao na wamiliki wa vyombo vya habari. Ni vigumu kumpata mwandishi wa habari atakayeandika kuhusu kashfa inayomhusisha mtoaji mkubwa wa matangazo ya biashara. Kulikuwa na mashtaka mahakamani kuhusu kampuni ya bia kutokana na kuzalisha bidhaa mbovu. Kila wakati chumba cha mahakama kilikuwa kimejaa waandishi wa habari, lakini hakuna habari yoyote iliyoandikwa au kutangazwa baada ya hapo. Vyombo vya habari havitatangaza ajali inayohusisha kampuni fulani za usafirishaji. Watoaji wakubwa wa matangazo ya biashara wana namna yao ya kuvinyamazisha vyombo vya habari. Mashirika machache yana sera inayowataka waandishi wa habari kusema zawadi na mambo mengine wanayopewa na watoa habari. ‘Lakini mara nyingi watasema tu, “Acha hili liwe siri yetu,”’ alisema mmoja wa washiriki. Alama: Alama za mshiriki mmoja mmoja: 1 Nchi inakidhi kiashiria 2 Nchi inakidhi vipengele vichache tu vya kiashiria 3 Nchi inakidhi vipengele kadhaa vya kiashiria 4 Nchi inakidhi vipengele vingi vya kiashiria 5 Nchi inakidhi vipengele vyote vya kiashiria Wastani wa alama: Alama ya miaka iliyopita: 52 ✓✓✓✓✓ ✓ ✓ ✓ ✓✓ ✓ 1.9 2006: n/a; 2008: n/a; 2010: 2; 2012: 1.5; 2015: 2.3 KIPIMO CHA VYOMBO VYA HABARI BARANI AFRIKA TANZANIA 2019 ✓