ENEO LA 4 4.4 Waandishi wa habari na wanahabari wengine wamejiunga kwenye vyama vya wafanyakazi na/ au vikundi vya kitaaluma, ambavyo vinawakilisha maslahi yao kikamilifu Umoja wa Waandishi wa Habari Tanzania haujafanya kazi tangu mwaka 2011 lakini umoja mpya, ambao ni Umoja wa Wafanyakazi Waandishi wa Habari Tanzania, ulikuwa ndo kwanza umeanzishwa. Pamoja na hilo, kuna Chama cha Waandishi wa Habari za Maendeleo Tanzania, ambacho ni muungano wa redio 35 za kijamii, ambacho kinapigania haki za waandishi wa habari wa redio za kijamii kama sehemu ya malengo yake. Vyama vya wafanyakazi Tanzania vimekuwa dhaifu. Kwa hivyo, vyama vya waandishi wahabari vina tabia ya kuangalia mambo mengine yanayohusu vyombo vya habari kama vile haki za vyombo vya habari, uhuru wa kujieleza na viwango vya kitaaluma. Kundi hili linajumuisha Muungano wa Klabu za Wanahabari Tanzania, Jukwaa la Wahariri Tanzania, Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Chama cha Waandishi wa habari za Michezo Tanzania, Taasisi ya Vyombo vya Habari Tanzania, Baraza la Vyombo vya Habari Tanzania na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika. Washiriki walisema kwamba baadhi ya vyama hutoza ada kubwa ya uanachama ambayo huwakatisha tamaa waandishi wa habari wachanga. Hata hivyo, vyama hivi vimekuwa na nguvu katika kuwakilisha maslahi ya waandishi wa habari. TAMWA inadhaniwa kuwa mojawapo ya vyama vya waandishi wa habari vyenye ushawishi zaidi na mara nyingi hutajwa kama taasisi ya kuigwa. Alama: Alama za mshiriki mmoja mmoja: 1 Nchi inakidhi kiashiria 2 Nchi inakidhi vipengele vichache tu vya kiashiria 3 Nchi inakidhi vipengele kadhaa vya kiashiria 4 Nchi inakidhi vipengele vingi vya kiashiria 5 Nchi inakidhi vipengele vyote vya kiashiria Wastani wa alama: Alama ya miaka iliyopita: 51 ✓✓ ✓ ✓ ✓✓✓ ✓ ✓ ✓ ✓ 2.3 2006: 2.2; 2008: 2.3; 2010: 2.2; 2012: 2.3; 2015: 2.5 KIPIMO CHA VYOMBO VYA HABARI BARANI AFRIKA TANZANIA 2019 ✓