ENEO LA 4

4.3 Ngazi za mishahara na mazingira ya jumla ya
utendaji kazi, ukiwemo usalama, kwa waandishi
wa habari na wanahabari wengine vinatosheleza
Washiriki walikisia kwamba takriban asilimia 80 ya waandishi wa habari Tanzania
hawana mikataba ya ajira, na hii ina maana kwamba wanapata ujira mdogo na
hawastahili mafao mengi ya kikazi. Hali ni mbaya zaidi kwenye vyombo binafsi
vya habari na ya kutisha zaidi kwenye redio za kijamii, ambapo wengi wao,
isipokuwa kwa wateule wachache hawana malipo maalum kabisa isipokuwa
posho kidogo. Katika kipindi cha miaka kumi iliyopita, kiwango cha mshahara
cha kuanzia ama hakijabadilika au kimeshuka, huku wengine wakilipwa viwango
vya chini hadi chini ya Shilingi za Kitanzania 350,000/= (sawa na Dola za
Kimarekani 150). Waandishi wa habari wa kujitegemea ni miongoni mwa wale
wanaolipwa kidogo zaidi, ambapo kwa wastani wanalipwa shilingi 10,000/= za
kitanzania (sawa na Dola 4 za Kimarekani) kwa kila habari, ikilinganishwa na
waandishi wa habari wa nje ambao hulipwa Dola za Kimarekani takriban 350
kwa kazi kama hiyo.
Washiriki walisema kwamba viwango vidogo vya mshahara wa kuanzia viliakisi
kiwango cha mshahara kwa kijana mwenye shahada ya kwanza nchi nzima,
ambacho ni wastani wa Shilingi 450,000/= za kitanzania (sawa na Dola 200 za
Kimarekani) kwa mwezi. Waandishi nguli wa habari wanapata zaidi ya hapo
kidogo. Waandishi wa habari waandamizi, mathalan, wanapata Shilingi za
Kitanzania takriban milioni moja (sawa na Dola za Kimarekani 434) kwa mwezi,
wakati wahariri wanapata kati ya Shilingi milioni 1.5 na million 5 za Kitanzania
(sawa na Doala kati ya 650 na 2,170 za kimarekani) kwa wastani. Nje na
mishahara, mazingira ya utendaji kazi ni mabaya kwa ujumla. Sharti la kisheria
linalowataka wamiliki wa vyombo vya habari kuwapa wafanyakazi wao kinga ya
bima na hifadhi ya jamii mara nyingi inakiukwa. Waandishi wasiolipwa mishahara
hawastahili kupewa bima na waandishi wote wa habari kwa ujumla hawana
kinga dhidi ya majanga ya kikazi. Washiriki walisimulia matukio ya mashambulio
ya kimwili (ikiwemo kutekwa) kwa waandishi wa habari, ili kushadidia ukosefu
wa kinga na usalama kwenye tasnia hii.

Alama:
Alama za mshiriki mmoja mmoja:
1

Nchi inakidhi kiashiria

2

Nchi inakidhi vipengele vichache tu vya kiashiria

3

Nchi inakidhi vipengele kadhaa vya kiashiria

4

Nchi inakidhi vipengele vingi vya kiashiria

5

Nchi inakidhi vipengele vyote vya kiashiria

Wastani wa alama:
Alama ya miaka iliyopita:

50

✓

✓

✓✓

✓✓

✓

✓✓✓✓✓

1.8
2006: n/a; 2008: n/a; 2010: 2.5; 2012: 1.8; 2015: 2.2

KIPIMO CHA VYOMBO VYA HABARI BARANI AFRIKA TANZANIA 2019

Select target paragraph3