ENEO LA 3 za kijamii ili kurusha vipindi vya TBC kama vile taarifa ya habari kwenye maeneo ya vijijini. Kwa vile luninga yake haitozwi ada, shirika linategemea sana mapato yatokanayo na matangazo ya biashara. Hata hivyo, washiriki waliona kwamba shinikizo la kufanya biashara lilikuwa na athari kidogo zaidi kwa TBC kuliko kuingiliwa kisiasa. Alama: Alama za mshiriki mmoja mmoja: 1 Nchi inakidhi kiashiria 2 Nchi inakidhi vipengele vichache tu vya kiashiria 3 Nchi inakidhi vipengele kadhaa vya kiashiria 4 Nchi inakidhi vipengele vingi vya kiashiria 5 Nchi inakidhi vipengele vyote vya kiashiria Wastani wa alama: Alama ya miaka iliyopita: ✓✓✓ ✓ ✓ ✓✓ ✓ ✓ ✓ ✓✓ 1.8 2006: n/a; 2008: n/a; 2010: 2.1; 2012: 2.5; 2015: 1.5 3.7 Chombo cha serikali kinatoa mchanganyiko wa vipindi na aina mchanganyiko ili kukidhi mahitaji ya makundi mbalimabali, ikiwamo maudhui ya kimaeneo na vipindi vyenye ubora na kuwakilisha maslahi ya umma TBC inatoa wigo mpana wa vipindi vinavyohusu mada anuai kuanzia siasa hadi mitindo. Hata hivyo, washiriki walisema kwamba vipindi vingi vinalenga kuelezea utendaji wa serikali na kuelemea upande chanya wa mamlaka badala ya kuangalia maslahi ya makundi yote. Ni kawaida kuona vipindi vinavyojadili mambo muhimu ya kisiasa kuondoka hewani ghafla. Mkutano wa hadhara wa kujadili rasimu ya katiba mpya, ikiwemo matangazo mbashara ya mijadala, uliondoka hewani ghafla baada ya dakika chache tu. Baadaye ulibadilishwa na maonesho ya mapishi. Na imekuwa kawaida kwa TBC kuwa hewani na vipindi ambavyo havina maslahi halisi kuliko kuwa na vipindi vya siasa ambavyo vinatoa maoni ambayo yanatofautiana na yale ya serikali. Baadhi ya washiriki walidai kwamba sauti kadhaa kinzani (hasa wanasiasa wa upinzani na watetezi wa haki za binadamu) wamezuiliwa kuonekana TBC. Chombo hiki pia chenyewe kimelazimika kuzuia vipindi vyenye wapenzi wengi hasa wanapoona kwamba hawawezi kudhibiti kile wanachoweza kukisema wazungumzaji waalikwa. 45 KIPIMO CHA VYOMBO VYA HABARI BARANI AFRIKA TANZANIA 2019