ENEO LA 3 inakipa chombo hiki wajibu wa kuutangazia umma na uhuru wa uhariri. Inaeleza kwamba: Kwa kuzingatia vipengele vya Sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, kutakuwa na Mkataba kati ya Shirika la Utangazaji Tanzania na Waziri ili kuliwezesha Shirika la Utangazaji Tanzania kuwa chombo cha utangazaji cha umma chenye wajibu wa kuhudumia watu wote. Mkataba huo utahakikisha kuwa Shirika la Utangazaji Tanzania linatekeleza malengo yake na kutumia mamlaka yake, linakuwa na uhuru wa kujieleza, uhandishi wenye ubunifu na vipindi bila kuingiliwa na serikali na wadau wengine. Washiriki walikuwa na maoni kwamba kiutendaji, TBC haikuwa na uhuru wa kiuhariri na kwa ujumla ilionekana kutumikia maslahi ya serikali iliyopo madarakani. Vilevile TBC inaonekana kama msemaji wa chama tawala na mara nyingi hudhihirisha hujuma zisizochujwa dhidi ya upinzani na sauti zenye ukinzani. Mmoja wa washiriki alisema kwamba watendaji na waandishi wa habari halikadhalika wanalazimika ‘kuufyata’ mara wanapoajiriwa TBC na kutekeleza sera za serikali, hata kama walikuwa wanahabari makini kabla ya kuteuliwa kushika nafasi walizo nazo. Washiriki walisema kwamba watendaji waliopita ambao walijaribu kuigeuza TBC ili kuendana na uhuru wa uhariri na kuruhusu mawazo mchanganyiko wamejikuta kwenye matatizo. Alama: Alama za mshiriki mmoja mmoja: 1 Nchi inakidhi kiashiria 2 Nchi inakidhi vipengele vichache tu vya kiashiria 3 Nchi inakidhi vipengele kadhaa vya kiashiria 4 Nchi inakidhi vipengele vingi vya kiashiria 5 Nchi inakidhi vipengele vyote vya kiashiria Wastani wa alama: Alama ya miaka iliyopita: ✓✓✓✓ ✓ ✓✓✓ ✓ ✓ ✓ ✓ 1.4 2006: n/a; 2008: n/a; 2010: n/a; 2012: n/a; 2015: 2.2 3.6 Chombo cha umma kinapewa fedha za kutosha kiasi cha kukilinda dhidi ya ushawishi wa kisiasa kupitia bajeti yake na dhidi ya ulazima wa kufanya biashara Kulingana na washiriki, TBC haikuwa inapewa fedha za kutosha na gawio la bajeti yake kwa mwaka kutoka wizarani linakidhi tu kulipa mishahara na mahitaji ya msingi ya uendeshaji- na hii inaathiri maendeleo kibiashara na mpangilio wa vipindi. Ili kuwafikia watu wengi, shirika limelazimika kuingia mkataba na redio 44 KIPIMO CHA VYOMBO VYA HABARI BARANI AFRIKA TANZANIA 2019