ENEO LA 3 Mshiriki mmoja alielezea jinsi ambavyo kipande maarufu kilitoweka kwenye taarifa ya habari: TBC ilikuwa na kipande cha makala kilichokuwa kinaitwa In Between the News, ambapo mtaalam au mchambuzi alikuwa anaalikwa kutoa maoni kuhusu matukio muhimu kwenye taarifa ya habari. Muda fulani, Rais aliwasamehe watu ambao walikuwa wametumia fedha za umma vibaya. Kabla ya kuwa hewani, aliambiwa, “Leo inabidi uongee vizuri kuhusu serikali na kuipongeza serikali kwa kufanya kitu kizuri”. Lakini alipokuwa hewani, alisema ilikuwa ni makosa kwa msamaha wa Rais kutolewa kabla ya wahusika kushtakiwa mahakamani ili kuwatia hatiani au kuwaachia huru. Kuanzia siku hiyo, kipindi cha In Between the News kilifutwa. Ili kuendelea kuwa hewani, TBC ina msururu wa matangazo ya tamthiliya, orodha ya miziki na vipindi vinavyoelezea ‘namna ya kuwa mzalendo na raia mwema au kuwa mke mzuri’. Alama: Alama za mshiriki mmoja mmoja: 1 46 Nchi inakidhi kiashiria 2 Nchi inakidhi vipengele vichache tu vya kiashiria 3 Nchi inakidhi vipengele kadhaa vya kiashiria 4 Nchi inakidhi vipengele vingi vya kiashiria 5 Nchi inakidhi vipengele vyote vya kiashiria ✓ ✓ ✓✓✓✓✓✓✓✓ ✓ Wastani wa alama: Alama ya miaka iliyopita: 2.4 2006: n/a; 2008: n/a; 2010: n/a; 2012: n/a; 2015: 2.6 Jumla ya alama kwenye sekta 3: 2.0 KIPIMO CHA VYOMBO VYA HABARI BARANI AFRIKA TANZANIA 2019 ✓