ENEO LA 3 3.4 Vyombo vya serikali/umma vinawajibika kwa umma kupitia bodi huru ambayo ina uwakilishi wa jamii kwa ujumla na ambayo imeteuliwa kwa njia iliyo huru na wazi. TBC ilianzishwa mwaka 2007 chini ya Sheria ya Mashirika ya Umma ya mwaka 2018. Inaongozwa na Mkurugenzi Mkuu na kusimamiwa na bodi ya wakurugenzi. Mkurugenzi mkuu pamoja na mwenyekiti wa bodi wanateuliwa na Rais, wakati wajumbe wengine wa bodi wanateuliwa na waziri, kila baada ya kipindi cha miaka mitatu. Wajumbe wa bodi hawana uhakika wa kumaliza kipindi chao kwa kuwa mamlaka ya uteuzi inaweza kutengua uteuzi wao kabla ya kumaliza muda wao. Washiriki walikuwa na maoni kwamba kwa kuangalia utaratibu wa uteuzi, bodi ya TBC isingeweza kudhaniwa kuwa huru. Bodi iliyopo iliteuliwa mwaka 2016.23 Pamoja na tathmini hasi ya uhuru wake, washiriki hawawafahamu wengi wa wajumbe wa bodi ya sasa na kwa hivyo wasingeweza kusema kama waliwakilisha jamii kwa ujumla. Alama: Alama za mshiriki mmoja mmoja: 1 Nchi inakidhi kiashiria 2 Nchi inakidhi vipengele vichache tu vya kiashiria 3 Nchi inakidhi vipengele kadhaa vya kiashiria 4 Nchi inakidhi vipengele vingi vya kiashiria 5 Nchi inakidhi vipengele vyote vya kiashiria Wastani wa alama: Alama ya miaka iliyopita: ✓ ✓ ✓ ✓ ✓ ✓✓✓ ✓ ✓✓ ✓ 1.6 2006: 1.5; 2008: 1.7; 2010: 1.9; 2012: 2.3; 2015: 2.1 3.5 Uhuru wa uhariri wa chombo cha umma/serikali dhidi ya ushawishi wa kisiasa unalindwa na sheria na unatumika kuhakikisha kwamba habari zinakuwa za haki na zenye uwiano na zenye kuakisi masuala yaliyopo Sheria iliyounda TBC inaeleza kwamba ‘itahimiza mtizamo wa kitanzania kwa kuwa na wigo mpana wa vipindi’. Katika Sehemu ya 7 (1-2), sheria ya TBC 23 Angalia taarifa mpya kupitia https://www.thecitizen.co.tz/News/Magufuli-appoints-new-TBC-board-chairman/18403403086330-rtfhwg/index.html. 43 KIPIMO CHA VYOMBO VYA HABARI BARANI AFRIKA TANZANIA 2019