ENEO LA 2 Alama: Alama za mshiriki mmoja mmoja: 1 Nchi inakidhi kiashiria 2 Nchi inakidhi vipengele vichache tu vya kiashiria 3 Nchi inakidhi vipengele kadhaa vya kiashiria 4 Nchi inakidhi vipengele vingi vya kiashiria 5 Nchi inakidhi vipengele vyote vya kiashiria Wastani wa alama: Alama ya miaka iliyopita: ✓✓ ✓✓ ✓ ✓ ✓✓ ✓✓ ✓ ✓ 3.2 2006: n/a; 2008: n/a; 2010: n/a ; 2012: n/a; 2015: 3.1 2.11 Nchi ina sera murua na kamilifu ya TEHAMA na/ au serikali inakuza na kutekeleza hatua ambazo zinakidhi mahitaji ya mawasiliano kwa umma, ikiwemo jamii za pembezoni Tanzania ni kinara katika kubuni na kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika ukanda wa Afrika ya Mashariki. Washiriki walisema kwamba Tanzania ni miongoni mwa nchi za mwanzo duniani kuunda teknolojia ya pochi jongefu na ina utaalam wa hali ya juu wa tiba ya masafa. Kwa kutumia mpango wa upatikanaji wa habari kwa wote, serikali hugharamia miradi ya kuunganisha maabara za kompyuta mashuleni na mafunzo kwa vijana. Washiriki walieleza kwamba serikali ilikuwa ikibuni njia za kusaidia mfumo wa teknolojia na wajasiriamali chipukizi kwenye teknolojia kwa kutoa fedha na mfumo mahsusi wa kodi kwa ajili ya kuwezesha mpango huo. Ushiriki wa serikali kwenye TEHAMA umeleta matokeo chanya kwenye sekta mbalimbali; hasa benki, biashara ya rejereja na biashara mtandao. Sera mpya ya TEHAMA ilichapishwa mwaka 2016 kwa lengo la ‘kubadlisha Tanzania kuwa na uchumi unaowezeshwa na TEHAMA, na ujuzi kupitia ubunifu na matumizi endelevu ya TEHAMA ili kumnufaisha kila mwananchi na biashara’.21 Washiriki walisema sera hiyo ilikuwa ya kimapinduzi na ilionesha utashi wa kisiasa wa kujenga jamii yenye ujuzi. 21 Sheria ya Taifa ya TEHAMA, 2016. 37 KIPIMO CHA VYOMBO VYA HABARI BARANI AFRIKA TANZANIA 2019