ENEO LA 2 michache tu iliyochunguzwa kila mwaka. Pamoja na hivyo, taarifa za habari kwa ujumla zimejikita maeneo ya mijini. Ni kampuni chache tu zenye waandishi wa habari kwenye maeneo ya pembezoni mwa nchi. Washiriki walieleza kwamba jamii za vijijini zinapewa nafasi wakati wa ziara za viongozi wakuu wa serikali kama vile ziara za mawaziri. Alama: Alama za mshiriki mmoja mmoja: 1 Nchi inakidhi kiashiria 2 Nchi inakidhi vipengele vichache tu vya kiashiria 3 Nchi inakidhi vipengele kadhaa vya kiashiria 4 Nchi inakidhi vipengele vingi vya kiashiria 5 Nchi inakidhi vipengele vyote vya kiashiria Wastani wa alama: Alama ya miaka iliyopita: ✓ ✓ ✓ ✓✓ ✓✓ ✓ ✓✓ ✓ ✓ 2.6 2006: 3.1; 2008: 2.3; 2010: 3.2; 2012: 3.3; 2015: 3.9 2.10 Watangazaji binafsi wanatoa vipindi vyenye viwango vinavyotakiwa vya maslahi ya umma Watangazaji binafsi wanatakiwa na sheria ‘kukuza uwelewa wa wananchi kuhusu masuala mbalimbali yenye maslahi ya kitaifa’ na ‘kutangaza na kuandika habari au masuala yenye umuhimu kitaifa kama itakavyoelekezwa na serikali.’19 Washiriki walisema watangazaji binafsi wanajitahidi kuzingatia matakwa haya lakini pia wanabanwa na hitaji la kuwafikia watu wengi ili kutengeneza vipindi vyenye maslahi kwa umma. Hata hivyo, inaonekana kuwepo na kutoelewana kati ya watangazaji na serikali kuhusu maana ya maslahi ya umma. Mathalan, washiriki walieleza kwamba watangazaji walitozwa faini kwa kutoa taarifa kuhusu madai ya kuwepo dosari wakati wa uchaguzi mdogo wa madiwani tarehe 26 Novemba 2017.20 19 Sheria ya Vyombo vya Habari Tanzania, Kifungu cha 7.2. 20 Mamala ya Mawasiliano Tanzania yalivitoza faini vituo vitano vya luninga jumla ya TZS 60 milioni ($27,000) kwa utangazaji ‘usiozingatia sheria na maadili”. Vituo hivyo vilirusha hewani tathmini iliyofanywa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kuhusu uchaguzi mdogo wa madiwani tarehe 26 Novemba, 2017, ambapo serikali iliona haukuzingatia sheria wala maadili. Ilipatikana kwa anuani hii: https://www.africanews.com/2018/01/03/tanzania-fines-tv-stations-forairing-human-rights-report// 36 KIPIMO CHA VYOMBO VYA HABARI BARANI AFRIKA TANZANIA 2019