ENEO LA 2 2.8 Vyombo vyote vya habari vinawakilisha mchanganyiko wa wanajamii kwa haki Tanzania ni jamii mchanganyiko ambayo ina makabila na lugha za kijamii zaidi ya 120. Hata hivyo, mchanganyiko huu hauakisiwi kwenye vyombo vya habari kwa kuwa sheria inazuia matangazo kwa lugha za kijamii. Kuruhusu matangazo kwa ‘Kiingereza fasaha na Kiswahili pekee’ ni sehemu ya mkakati wa serikali wa kudumisha umoja wa kitaifa na kuzuia uwezekanao wa makabila machache kuwa na nguvu kuliko mengine. Hata hivyo, washiriki walikosoa njia hiyo kama isiyo na ushahidi. ‘Hii inamkosesha mtanzania wa kawaida sauti kwenye vyombo vya habari.’ ‘Sisi ni nchi yenye mchanganyiko lakini bado tuko mbali katika kuukubali mchanganyiko na wingi wetu.’ Washiriki walisema pamoja na lugha, kulikuwa na matatizo kuhusu namna ambavyo makundi mbalimbali ya kijamii (hasa wale wachache) yanawakilishwa kwenye vyombo vya habari: kwa ujumla vyombo vya habari hutengeneza imani potofu kuhusu Waarabu na Wahindi wa Tanzania. Aidha, ni vipindi vichache sana huwalenga watu wenye ulemavu. Matumizi ya lugha ya alama kwenye luninga ni nadra na hakuna magazeti yanayotumia nukta nundu. Alama: Alama za mshiriki mmoja mmoja: 1 Nchi inakidhi kiashiria 2 Nchi inakidhi vipengele vichache tu vya kiashiria 3 Nchi inakidhi vipengele kadhaa vya kiashiria 4 Nchi inakidhi vipengele vingi vya kiashiria 5 Nchi inakidhi vipengele vyote vya kiashiria Wastani wa alama: Alama ya miaka iliyopita: ✓ ✓ ✓ ✓ ✓✓✓ ✓✓ ✓✓✓ 2.2 2006: n/a; 2008: n/a; 2010: 2.6 ; 2012: 2.8; 2015: 3 2.9 Vyombo vya habari vinagusa maeneo yote ya kiuchumi, kiutamaduni, kisiasa, mitazamo ya kitaifa na kimaeneo, ikiwa ni pamoja na kwa njia ya taarifa za kiuchunguzi Tanzania itafanya uchaguzi mkuu mwaka 2020. Wakati wa AMB hii (takriban mwaka mmoja kabla ya upigaji kura) washiriki walisema kwamba kulikuwa na habari chache sana kuhusu uchaguzi huo. Walieleza kwamba ufinyu wa habari kuhusu uchaguzi unaokaribia unaonesha kupungua kwa kasi kwa habari za kisiasa kwa ujumla. Kutokana na athari za kuogofya za fursa za kisiasa zinazozidi kudorora, waandishi wa habari wamegeukia kwenye mada ambazo zinadhaniwa kuwa na hisia kidogo kama vile maslahi ya kibinadamu, utamaduni na shughuli za serikali. Uhandishi wa habari za kiuchunguzi pia umeathirika, na ni miradi 35 KIPIMO CHA VYOMBO VYA HABARI BARANI AFRIKA TANZANIA 2019