ENEO LA 2 2.7 Vyombo vyote vinazingatia usawa kwa jinsia zote Pamoja na mafanikio yaliyopatikana kwa miaka mingi, wanaume bado wanatamalaki kwenye taarifa za habari. Washiriki walisema kwamba maisha ya kijamii na kiutamaduni ambayo yanawafanya wanawake waonekane kama kivuli kwenye jamii kwa kiasi fulani yanasababisha uchache wa wanawake kwenye vyombo vya habari. ‘ni wachache kati yao wako radhi kuongea, hata wanapoombwa kufanya mahojiano.’ Uwakilishi wa wanawake kwenye vyombo vya habari pia unaakisi jamii ambayo kwa kiasi kikubwa imekaa kimfumo dume. Kwa ujumla, wanaume wanatawala anga la umma na kudhibiti habari na mada za kijamii na wigo wa habari. Habari zinazohusu wanawake zinapopenya kwenye vyombo vya habari, zinawasilishwa kupitia lensi ya wanaume na huwa zenye msisimuko na kudhalilisha. Washiriki walieleza kwamba vyombo vya habari pia huwa na tabia ya kuwabagua wanawake kwa kificho. Wakati wa kampeni za kisiasa, mathalan, wagombea wa kiume huwa wanapata muda mwingi zaidi kuliko wenzao wa kike. ‘Kuna wanawake wachache wenye nguvu ambao wako radhi kuongea lakini ambao hawapatiwi fursa,’ alisema mmoja wa washiriki. Vyombo vya habari vimeshindwa kukosoa imani potofu dhidi ya wanawake na badala yake vimeshiriki kuziendeleza imani hizo: Rais alipowakataza wasichana wenye ujauzito kuendelea na masomo, vyombo vya habari viliikimbilia habari hiyo bila kuhoji utata katika sera hiyo. Wanapotoa habari zinazohusu wanawake, wanaonekana kama wahanga. Habari zinakuwa za udhalilishaji na zenye imani potofu. Vyombo vichache vya habari vimefanya mabadiliko ya makusudi ya sera ili kuongeza sauti za wanawake. Mathalan, waandishi wa habari wa ndani na watangazaji wa Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) wanatakiwa kujumuisha wanawake kwenye taarifa zao na vipindi vyao. Redio za kijamii pia zimefanya mabadiliko kwa miaka mingi ili kuongeza sauti za wanawake na mada zenye maslahi kwa wanawake. Alama: Alama za mshiriki mmoja mmoja: 1 Nchi inakidhi kiashiria 2 Nchi inakidhi vipengele vichache tu vya kiashiria 3 Nchi inakidhi vipengele kadhaa vya kiashiria 4 Nchi inakidhi vipengele vingi vya kiashiria 5 Nchi inakidhi vipengele vyote vya kiashiria Wastani wa alama: Alama ya miaka iliyopita: 34 ✓ ✓ ✓ ✓ ✓✓✓ ✓ ✓✓✓✓ 2.1 2006: n/a; 2008: n/a; 2010: 2.7; 2012: 3.4; 2015: 2.6 KIPIMO CHA VYOMBO VYA HABARI BARANI AFRIKA TANZANIA 2019