ENEO LA 2

habari kwa lengo la kukuza na kuwezesha kampuni zao weneyewe – na
hivyo kusahau maudhui yenye maslahi mapana ya kijamii.
Washiriki walisema kwamba eneo mojawapo la tatizo hilo ni kushindwa kwa
Sheria ya Vyombo vya Habari kushughulikia tatizo la msongamano wa vyombo
vya habari. Washawishi wa vyombo vya habari wameshindwa kwa miaka mingi
kushawishi mamlaka kubadilisha sheria inayomruhusu mmiliki mmoja kumiliki
vyombo anuai vya habari. Matokeo yake, tasnia ya habari inadhibitiwa na watu
wasiofikia hata watano pamoja na washirika wao.

Alama:
Alama za mshiriki mmoja mmoja:
1

Nchi inakidhi kiashiria

2

Nchi inakidhi vipengele vichache tu vya kiashiria

3

Nchi inakidhi vipengele kadhaa vya kiashiria

4

Nchi inakidhi vipengele vingi vya kiashiria

5

Nchi inakidhi vipengele vyote vya kiashiria

Wastani wa alama:
Alama ya miaka iliyopita:

✓

✓
✓

✓

✓

✓

✓

✓

✓✓

✓

✓

2.6
2006: 1.6; 2008: 2.4; 2010: 1.7; 2012: 2.7; 2015: 2.8

2.6 Serikali inakuza wigo mpana wa mandhari ya
vyombo vya habari yenye vyanzo endelevu
kiuchumi na huru
Tanzania ina wigo mpana ya vyombo vya habari ambapo vyanzo anuai vinatoa
huduma ya habari kwa makundi anuai. Hata hivyo, washiriki walisema kwamba
hayo si matokeo ya sera ya serikali. Kinyume chake, hazina ya sheria za kufisha
imetumiwa kuhujumu mazingira ya kuwepo kwa vyombo vya habari endelevu
kiuchumi na huru. Ada za leseni kwa vyombo vyote vya habari, mathalan, ni
kubwa na zinakatisha tamaa. Mali ghafi zinazotumiwa na vyombo vya habari
hazina msamaha wa kodi na hata redio za kijamii lazima zilipe ada kubwa ya
leseni kila mwaka.

Alama:
Alama za mshiriki mmoja mmoja:
1

Nchi inakidhi kiashiria

2

Nchi inakidhi vipengele vichache tu vya kiashiria

3

Nchi inakidhi vipengele kadhaa vya kiashiria

4

Nchi inakidhi vipengele vingi vya kiashiria

5

Nchi inakidhi vipengele vyote vya kiashiria

Wastani wa alama:
Alama ya miaka iliyopita:

33

✓✓✓✓✓
✓

✓✓✓✓

✓✓

2.5
2006: n/a; 2008: n/a; 2010: 1.8 ; 2012: 1.3; 2015: 2.8

KIPIMO CHA VYOMBO VYA HABARI BARANI AFRIKA TANZANIA 2019

Select target paragraph3