ENEO LA 2

makampuni na makampuni kuunda makampuni mengine kiasi kwamba kujua
ni nani hasa yuko nyuma ya chombo cha habari, ni lazima ufanye uchunguzi
wa kina,’ alisema mmoja wa washiriki. Mshiriki mwingine aliongezea kwamba
inawezekana kwamba mmiliki halisi wa vyombo vya habari akawatumia watu
wengine na makampuni kama watangulizi.

Alama:
Alama za mshiriki mmoja mmoja:
1

Nchi inakidhi kiashiria

2

Nchi inakidhi vipengele vichache tu vya kiashiria

3

Nchi inakidhi vipengele kadhaa vya kiashiria

4

Nchi inakidhi vipengele vingi vya kiashiria

5

Nchi inakidhi vipengele vyote vya kiashiria

Wastani wa alama:
Alama ya miaka iliyopita:

✓✓

✓✓

✓
✓✓✓

✓✓

✓✓

2.8
2006: n/a; 2008: n/a; 2010: n/a; 2012: n/a; 2015: 3.8

2.5 Sheria zinajitosheleza kuendeleza ushindani na
kuzuia msongamano na kuhodhi vyombo vya
habari
Sheria ya Ushindani Huru ya mwaka 2003 inapaswa kuzuia mrundikanao na
kuhodhi katika sekta mbalimbali, ikiwemo sekta ya habari. Hata hivyo, kiutendaji,
mrundikano wa vyombo vya habari ni mkubwa Tanzania. Utafiti uliofanywa
mwaka 201818 na MCT na Waandishi wa Habari Wasio na Mipaka ulionesha
kwamba vyombo vya habari Tanzania vilikuwa vimeodhiwa na watu wachache
sana.
Utafiti huo ulibainisha kwamba:
Baadhi ya makundi makubwa ya vyombo vya habari yanamilikiwa na
wamiliki ambao hudhibiti makampuni yenye wigo mpana wa maslahi
kwenye sekta nyingine za biashara. Mathalan, marehemu Dr. Reginald
Mengi, ambaye ni mwanzilishi wa IPP Media Group, alikuwa amejikita
kwenye biashara ya vinywaji vya chupa, kwenye bidhaa za nyumbani
na bidhaa za urembo na uchimbaji madini. Vile vile alikuwa na nia ya
kuwekeza kwenye uchimbaji wa mafuta na gesi, viwanda vya magari
na madawa. Mfano mwingine ni ule wa Said Salim Bakhresa, bilionea
aliyejiendeleza mwenyewe na aliyeanzisha Azam TV, ambayo inalipiwa
Afrika ya Mashariki nzima. Kundi lake la Bakhresa Group kwa leo ni
miongoni mwa taasisi kubwa zaidi Afrika ya Mashariki, ikijumuisha
biashara ya vyakula na vinywaji, ufungashaji, huduma za usafiri wa majini
na biashara ya mafuta ya magari. Kuna hatari ya wamiliki wa vyombo
vya habari wenye maslahi anuai ya kibiashara kutumia vyombo vyao vya
18 Angalia ‘Nani Anamiliki Vyombo vya Habari Tanzania?’ Inapatikana mtandaoni kwa anuani hii: https://rsf.org/en/reports/
who-owns-media-tanzania. Mara ya mwisho ilipatkana tarehe 29 Mei 2019.

32

KIPIMO CHA VYOMBO VYA HABARI BARANI AFRIKA TANZANIA 2019

Select target paragraph3