ENEO LA 2 2.3 Uhuru wa wahariri wa magazeti na vyanzo vya habari mitandaoni zinazochapishwa na mamlaka za umma unalindwa vya kutosha dhidi ya kuingiliwa kisiasa kusiko kwa lazima Tanzania ina magazeti mawili yanayomilikiwa na serikali, ambayo ni Daily News na Habari Leo. Magazeti haya mawili na matoleo yake ya matandaoni kwa kiasi kikubwa yanaonekana kama kipaza sauti cha serikali iliyoko madarakani na sehemu ya nyenzo ya dola. Matokeo yake ni kwamba havina uhuru wa uhariri. Washiriki waliezea utamaduni wa kuegemea upande mmoja, uchujaji habari/ kujichuja na uhandishi wa ‘mapambazuko’ kwenye magazeti yanayomilikiwa na serikali. Pamoja na mambo mengine, wahariri na waandishi wa habari wa Daily News na Habari Leo wana utaratibu wa kuzima habari ambazo siyo rafiki kwa serikali na kunyamazisha sauti za watu wenye mawazo kinzani. Uchambuzi wa maudhui kwenye gazeti la Daily News mwaka 2018 ulionesha kwamba gazeti hilo halikuandika habari yoyote ya kuikosoa serikali kwa mwaka mzima. Mmoja wa wanajopo alisema kwamba, ‘Unapokubali ajira Daily News, unajua moja kwa moja kwamba kuna habari ambazo huwezi kugusa.’ Ingawa washiriki walikubaliana kwamba magazeti yanayomilikiwa na serikali hayana uhuru wa uhariri, baadhi yao walidhani kwamba kukosekana kwa uhuru kunaweza kusiwe na tatizo. Mmoja wa washiriki alisema kwa hisia kwamba kama sehemu ya chombo cha serikali, magazeti yanayomilikiwa na serikali yanapaswa kuangaliwa kama vyombo vilivyoko kwenye mikono ya mamlaka ili kuchagiza utendaji wa serikali. Alama: Alama za mshiriki mmoja mmoja: 1 Nchi inakidhi kiashiria 2 Nchi inakidhi vipengele vichache tu vya kiashiria 3 Nchi inakidhi vipengele kadhaa vya kiashiria 4 Nchi inakidhi vipengele vingi vya kiashiria 5 Nchi inakidhi vipengele vyote vya kiashiria Wastani wa alama: Alama ya miaka iliyopita: ✓✓ ✓✓ ✓ ✓ ✓✓ ✓ ✓✓ ✓ 1.9 2006: 2.4; 2008: 1.8; 2010: 1.9; 2012: 2.3; 2015: 1.8 2.4 Uwazi wa umiliki wa vyombo vya habari unatolewa na kulindwa na sheria Umiliki wa vyombo vya habari Tanzania unathibitika kiraisi kwa vile mamlaka yana orodha ya wamiliki wa makampuni na wadau chini ya Sheria ya Makampuni. Hata hivyo, washiriki walisema kwamba daftari la umiliki wa makampuni linaweza lisioneshe wamiliki halisi wa vyombo vya habari. ‘Watu wanaweza kuunda 31 KIPIMO CHA VYOMBO VYA HABARI BARANI AFRIKA TANZANIA 2019