ENEO LA 1 1.10 Asasi ya kiraia kwa ujumla na makundi ya ushawishi wa vyombo vya habari yanafanya jitihada chanya kusaka uhuru wa vyombo vya habari Asasi za kiraia Tanzania kwa ujumla zinadhaniwa kuwa na muundo mzuri na zina nguvu. Mara nyingi, zinaungana na vyombo vya habari kwenye mambo yanayohusu uandishi wa habari kama vile upatikanaji wa habari na kuharamisha habari zinazodaiwa kuwa kashfa. Muungano wa Haki ya Habari (CORI) unajulikana sana kwa kuhamasisha taasisi zenye mlengo unaofanana kwa ajili ya kuchagiza madai ya kimkakati na kushawishi dhidi ya sheria kandamizi za vyombo vya habari. Taasisi nyingine ambazo mara nyingi huchagiza masuala ya uhandishi wa habari ni pamoja na Muungano wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) na Jukwaa la Umoja wa Asasi za Kiraia Afrika Mashariki (EACSOF). Washirki walisema kwamba mashirika yasiyo ya kiserikali yalitumia mbinu anuai na kuainisha mambo kadha wa kadha, ila mara nyingi sana yanashiriki kwenye harakati zilizoratibiwa. Harakati kama hizo za NGOs nje ya vyombo vya habari hujaziliza jitihada na ushawishi unaofanywa na taasisi za vyombo vya habari. Hizi pia zinaonekana kuwa hai na zenye nguvu katika kuweka msukumo kwa haki za vyombo vya habari. Taasisi zilizo mstari wa mbele ni pamoja na Jukwaa laWahariri Tanzania, Baraza la Habari Tanzania (MCT), Taasisi ya Vyombo vya Habari Tanzania (TMF), Shirika la Habari za Maendeleo Tanzania (TADIO), THRDC, Umoja wa Klabu za Wanahabari Tanzania na Taasisi ya Vyombo vya Habari Afrika ya Kusini (MISA). Alama: Alama za mshiriki mmoja mmoja: 1 Nchi inakidhi kiashiria 2 Nchi inakidhi vipengele vichache tu vya kiashiria 3 Nchi inakidhi vipengele kadhaa vya kiashiria 4 Nchi inakidhi vipengele vingi vya kiashiria 5 Nchi inakidhi vipengele vyote vya kiashiria Wastani wa alama: Alama ya miaka iliyopita: ✓✓✓✓✓ ✓ ✓✓ ✓✓ ✓ ✓ 4.2 2006: 2.8; 2008: 2.7; 2010: 3.2; 2012: 4.1; 2015: 4.1 1.11 Sheria za vyombo vya habari zinatokana na mazungumzo mujarabu kati ya taasisi za serikali, wananchi na makundi mengine Kwa kiasi kikubwa, mchakato wa kutunga sheria Tanzania umehodhiwa na serikali kuu na mara nyingi hukosa mchango wa kutosha wa wadau wengine 26 KIPIMO CHA VYOMBO VYA HABARI BARANI AFRIKA TANZANIA 2019