ENEO LA 1 wa kisiasa na kijamii. Kwa mujibu wa washiriki, panapokuwa na majadiliano, mawazo ambayo hayaoani na mtizamo wa serikali hayazingatiwi. Katika hali ya kupindukia, serikali hutumia makundi na watu binafsi nje ya mfumo rasmi wa kisheria kushadidia msimamo wa serikali wakati wa vikao vya majadiliano- na hivyo kuzima sauti za watu wenye mawazo kinzani. Utamaduni huu wa utungaji wa sheria unadhihirika pia kwenye sheria zinazohusu vyombo vya habari. Ili kuzuia mijadala (hata ndani ya bunge), mara nyingi mamlaka hutumia nyenzo inayoitwa ‘hati ya dharura’, ambayo hutumiwa kuharakisha kupitisha sheria kwa kupunguza ngazi za uchambuzi ambazo mswada unatakiwa kupitia kwenye bunge. Miaka michache iliyopita, sheria mbili zenye athari za moja kwa moja kwa vyombo vya habari zimepitishwa kwa kutumia mtindo huu. Sheria hizo ni ile ya Makosa ya Mtandaoni na ile Sheria ya Takwimu. Washiriki walitabanaisha kwamba wakati mwingine majadiliano husababisha kuwepo kwa sheria mbaya zaidi za vyombo vya habari- watetezi wa vyombo vya habari walishindwa kuzuia kutungwa kwa Sheria ya Vyombo vya Habari na inawezekana wakawa wamesaidia kuharakisha matumizi yake. Hatua dhahiri inayoonesha kutoheshimiwa kwa madai yao, ni kwamba Sheria ya Vyombo vya Habari ilitiwa sahihi kuwa sheria kamili siku moja baada ya kikao kati ya makundi ya watetezi wa vyombo vya habari na mamlaka husika, ambapo watetezi wa vyombo vya habari walikuwa wametoa mapingamizi dhidi ya sheria hiyo. Ushawishi wa umma kwenye mchakato wa kutunga sheria ulizaa matunda kwenye matukio machache. Sheria ya Upatikanaji wa Habari, mathalan, ilisimamishwa kwa mwaka mmoja kutokana na malalamiko ya wananchi. Washiriki walisema kwamba washawishi wa vyombo vya habari walifanikiwa kuondoa kifungu ambacho kinapiga marufuku kutumia taarifa zilizopatikana kupitia ombi la FOI kwa umma. Kifungu hiki kilirithiwa na kifungu kingine chenye unafuu zaidi ingawa bado kandamizi, ambacho kiliharamisha kubadili maudhui ya habari zilizopatikana kutoka kwa ombi la FOI. Alama: Alama za mshiriki mmoja mmoja: 27 1 Nchi inakidhi kiashiria 2 Nchi inakidhi vipengele vichache tu vya kiashiria 3 Nchi inakidhi vipengele kadhaa vya kiashiria 4 Nchi inakidhi vipengele vingi vya kiashiria 5 Nchi inakidhi vipengele vyote vya kiashiria ✓✓ ✓ ✓ ✓ ✓✓ ✓ ✓ ✓✓✓ Wastani wa alama: Alama ya miaka iliyopita: 2.0 2006: n/a; 2008: n/a; 2010: 2.6; 2012: 3.8; 2015: 1.7 Jumla ya alama kwenye sekta 1: 2.2 KIPIMO CHA VYOMBO VYA HABARI BARANI AFRIKA TANZANIA 2019