ENEO LA 1 1.9 Serikali haioneshi nia ya kuzuia au kuchuja habari za mtandaoni isipokuwa kwa matakwa ya kisheria ambayo yanaruhusu makatazo yanayohusiana na maslahi halali na ambayo ni yalazima katika jamii ya kidemokrasia na ambayo yanatumika na mahakama huru Washiriki walieleza kwamba kwa sababu ya sifa mbaya ya mamlaka kwa kujaribu kuzuia uhuru wa habari, kulikuwa na uwezekano mkubwa kwamba serikali ingechukua hatua madhubuti ili kuzuia au kuchuja habari mtandaoni. Pamoja na kukosekana kwa ushahidi thabiti, maoni haya yanaonekana kuwa yamejikita zaidi kwenye uelewa wa wananchi kwa sababu ya sera ya serikali. Mathalan, hatua ya serikali ya kuunganisha Moduli ya Utambulisho wa Mtumiaji (SIM) wa simu za mkononi na taarifa binafsi za mmiliki wa simu ya mkononi umesababisha wasiwasi kwamba serikali ilikuwa na nia ya kufanya udukuzi mkubwa wa taarifa za raia. Mmoja wa washiriki alidai kwamba kwa msaada wa China, kikosi cha taifa cha makosa ya mtandaoni kilikuwa kimepata maarifa na uwezo mkubwa wa kuingilia tovuti na kuzuia kusambaa kwa habari lengwa katika mtandao. Kipindi cha uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, mawasiliano kupitia Jamii Forums, jukwaa la mjadala mtandaoni na jukwaa la kupuliza filimbi, ilizuiliwa kwa njia ya ajabu kwa saa 24, na kusababisha wananchi kudhani kwamba mtandao huo ulikuwa umetekwa na wataalam kutoka Ukraine au Urusi kwa niaba ya mamlaka. Pamoja na ishara hizo za wazi za kuingilia habari mitandaoni, uhusika wa moja kwa moja wa mamlaka unaonekana wa kudhaniwa zaidi kuliko wa kuthibitika. Alama: Alama za mshiriki mmoja mmoja: 1 Nchi inakidhi kiashiria 2 Nchi inakidhi vipengele vichache tu vya kiashiria 3 Nchi inakidhi vipengele kadhaa vya kiashiria 4 Nchi inakidhi vipengele vingi vya kiashiria 5 Nchi inakidhi vipengele vyote vya kiashiria Wastani wa alama: Alama ya miaka iliyopita: 25 ✓ ✓✓✓ ✓ ✓✓✓ ✓ ✓ ✓ 2.2 2006: n/a; 2008: n/a; 2010: 3.3; 2012: 4.5; 2015: 3.3 KIPIMO CHA VYOMBO VYA HABARI BARANI AFRIKA TANZANIA 2019 ✓