ENEO LA 1 1.8 Tovuti, blogu na majukwaa mengine ya kidijitali hayahitaji kusajiliwa na; au kupata idhini kutoka kwa mamlaka za serikali Njia za mawasiliano mtandaoni (kwa tafsiri ya redio za mtandaoni, Luninga za mtandaoni, blogu na vyanzo vingine vya mtandaoni) zinawajibika kupata leseni ya miaka mitatu ambayo hutolewa na TCRA. Sheria za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (maudhui ya mtandaoni) ya mwaka 2018 zinaweka ada ya awali kwa huduma za mtandaoni ya shilingi za kitanzania milioni moja (sawa na Dola za Kimarekani 453, kabla ya ada ya mwaka na ada ya kuongeza muda wa leseni ya kiwango sawa na hicho. Tozo nyinginezo ni pamoja na ada ya maombi ya leseni ya shilingi za kitanzania 100,00015 (sawa na US$43). Hata pale ambapo masharti ya kifedha yametmizwa, sheria inaipa TCRA mamlaka ya kufuta leseni ya chombo cha mtandaoni ‘endapo vigezo na masharti yatakiukwa’. Sheria hizi zinaonekana kuwa kandamizi na zenye lengo la kudhoofisha majukwaa yaliyopo ya kujieleza kwa uhuru. Zinaathiri majukwa ya mtandaoni na watumiaji wa mitandao ya kijamii na, kwa maelezo ya mmoja wa washiriki, wamiliki na watumiaji wa blogu Tanzania wanaoishi nje ya nchi pia. Alama: Alama za mshiriki mmoja mmoja: 1 Nchi inakidhi kiashiria 2 Nchi inakidhi vipengele vichache tu vya kiashiria 3 Nchi inakidhi vipengele kadhaa vya kiashiria 4 Nchi inakidhi vipengele vingi vya kiashiria 5 Nchi inakidhi vipengele vyote vya kiashiria Wastani wa alama: Alama ya miaka iliyopita: ✓ ✓✓✓✓✓✓✓✓✓✓✓ 1.1 2006: n/a; 2008: n/a; 2010: 3; 2012: 4.8; 2015: 4.7 15 Rasimu ya pili ya Sheria ya Mwasiliano ya Kielektroniki na Posta (mtandaoni) ya mwaka 2081, ambayo pia iliweka viwango vya ada ya leseni kwa matangazo ya redio na luninga mtandaoni. 24 KIPIMO CHA VYOMBO VYA HABARI BARANI AFRIKA TANZANIA 2019