ENEO LA 1 Kuna sababu nyingi zinazofanya kuwe na mtizamo hasi. Kubwa kuliko zote inaonekana kuwa kutokujitambua miongoni mwa wamiliki wa habari, kama vile manispaa, Wakurugenzi Watendaji wa Wilaya (DEDs) na maafisa habari kuhusu majukumu yao. Mmoja wa washiriki alielezea hali hii kama ifuatavyo, ‘Wakati mwingine, afisa habari anaweza akakuambia yeye si mzungumzaji wa Mkurugenzi Mtendaji. Pamoja na kwamba sheria inampa mamlaka afisa habari kutoa habari na kuwasaidia wale wanaotafuta habari, baadhi yao bado watakuambia kwamba wanahitaji idhini ya wakuu wao wa kazi au DED. ‘Wakati huo huo, baadhi ya wilaya zimeacha utaratibu wa kutoa taarifa kwa umma kwa kutumia njia nyingine zilizokuwa zinatumia hapo kabla, kwa sababu wanahisi kwamba taarifa zote kwa sasa lazima zitolewe na maafisa habari.’ Kwa kiasi kikubwa, washiriki waliona kwamba Sheria ya Upatikanaji wa Habari ilikuwa imeirudisha nchi nyuma badala ya kuisaidia kusonga mbele. Walibainisha kwamba umma haukuwa tena na uwezo wa kupokea taarifa kwa muda muafaka kama ilivyokuwa hapo kabla wakati wilaya zilipokuwa na utaratibu wa kutumia viongozi wa mtaa ili kuwasilisha taarifa kwa wapiga kura. Kwa kuzingatia wajibu finyu wa kisheria wa kuheshimu maombi ya taarifa, mamlaka za umma zinatoa tu taarifa ambazo zinakidhi maslahi yao, ambapo maslahi haya yanakuwa hayana wigo mpana. Hata hivyo, kwa sababu za mahitaji ambatizi, baadhi ya taasisi za umma kama vile Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) mara nyingi hutoa taarifa kwa umma kwa wakati. Alama: Alama za mshiriki mmoja mmoja: 1 Nchi inakidhi kiashiria 2 Nchi inakidhi vipengele vichache tu vya kiashiria 3 Nchi inakidhi vipengele kadhaa vya kiashiria 4 Nchi inakidhi vipengele vingi vya kiashiria 5 Nchi inakidhi vipengele vyote vya kiashiria Wastani wa alama: Alama ya miaka iliyopita: 23 ✓✓ ✓ ✓ ✓✓ ✓ ✓ ✓ ✓ ✓ 2.2 2006: 1.1; 2008: 1.3; 2010: 1.6; 2012: 2.5; 2015: 1.6 KIPIMO CHA VYOMBO VYA HABARI BARANI AFRIKA TANZANIA 2019 ✓