ENEO LA 1 1.6 Vyanzo vya siri vya habari vinalindwa na sheria na/au mahakama Tanzania haina sheria mahsusi inayotoa ulinzi kwa vyombo vya habari. Sheria kandamizi kama vile [Sheria ya Mpiga Filimbi na Shaidi] hazitumiki moja kwa moja kulinda vyanzo vya siri vya habari. Hata hivyo, washiriki walisema kwamba wananchi kwa ujumla wanajua kwamba waandishi wa habari hawatakiwi kuweka bayana vyanzo vya siri vya habari kama kitu cha kawaida katika uhandishi wa habari. Kwa hivyo, kwa kuzingatia kanuni hizi zinazokubalika kwa ujumla, waandishi wa habari na taasisi za habari mara nyingi huwa wanaamua kulinda vyanzo vyao vya habari. Pamoja na hayo, kukosekana kwa kinga ya kisheria mara nyingi husababisha bugudha kwa waandishi wa habari. Washiriki walisema kwamba ilikuwa kawaida kwa waandishi wa habari kuteswa na kubinywa kwa njia nyinginezo ili wabainishe vyanzo vyao vya habari. Mathalan, waendeshaji wa Jamii Forums, jukwaa la mtandaoni ambalo huwawezesha wananchi ‘kuthubutu kuongea kwa uhuru’, mara nyingi limekuwa kwenye mbinyo ili kubainisha utambulisho wa wachangiaji wanaotumia majina bandia. Kwa mtazamo wa washiriki na taarifa za habari, mwaka 2016 askari polisi waliwakamata waendeshaji wa jukwaa hilo, Maxence Melo Mubyazi na Micke Williams na kuwafungulia mashtaka kwa kuzuia haki kutendeka kwa kukataa kutoa taarifa za wanachama wao.14 Wawili hao walishtakiwa chini ya Sheria ya Makosa ya Kimtandao na endapo watatiwa hatiani, watakabiliwa na adhabu ya kulipa hadi Shilingi milioni tatu za Kitanzania; sawa na Dola 1,300 za Kimarekani, kifungo cha muda usiopingua mwaka mmoja jela, au adhabu zote mbili. Waanzilishi hao wa ‘Jamii Forums wamekuwa wakienda na kurudi mahakamani kwa vile mamlaka zinalazimisha kupewa taarifa kuhusu wanachama.’ Alama: Alama za mshiriki mmoja mmoja: 1 Nchi inakidhi kiashiria 2 Nchi inakidhi vipengele vichache tu vya kiashiria 3 Nchi inakidhi vipengele kadhaa vya kiashiria 4 Nchi inakidhi vipengele vingi vya kiashiria 5 Nchi inakidhi vipengele vyote vya kiashiria Wastani wa alama: Alama ya miaka iliyopita: ✓✓ ✓ ✓✓✓✓ ✓✓ ✓✓✓ 2.3 2006: 1.6; 2008: 2.3; 2010: 1.8; 2012: 1.3; 2015: 1.2 14 Angalia kwa mfano taarifa ya habari ya BBC ya tarehe 16 Disemba 2016. Inapatikana mtandaoni kwa anuani hii://www. bbc.com/news/world-africa-38341151. Mara ya mwisho ilipatikana tarehe 22 Mei 2019. 21 KIPIMO CHA VYOMBO VYA HABARI BARANI AFRIKA TANZANIA 2019