ENEO LA 1

masharti yaliyowekwa’.12 Masharti ya leseni ya magazeti yameelezwa kwenye
Kifungu cha 7 hadi cha 16 cha Kanuni ya Huduma za Magazeti ya Mwaka 2017.
Kanuni hii inaeleza kwamba leseni itaongezewa muda kila mwaka, na waombaji
wanapaswa kulipa ada ya awali pamoja na ada ya mwaka ya kuongeza muda wa
leseni (Kifungu cha 12 & 13).
Washiriki walisema kwamba mfumo wa utoaji leseni ulitengenezwa maksudi ili
kuendeleza udhibiti wa serikali dhidi ya vyombo vya habari kwa njia ya maandishi,
hasa kwa kutumia mamlaka isivyo ili kukataa kutoa leseni, na kufungia au
kufuta leseni. Wanajopo walikuwa na hisia kwamba sharti la kuongeza muda
wa leseni kwa mwaka liliiwezesha serikali kuweka kitanzi cha kudumu kwenye
shingo ya vyombo vya habari vya kimaandishi na kuviweka chini ya udhibiti.
‘Gazeti linapokuwa limepewa leseni, serikali hulitupia macho, ‘alisema mmoja
wa washiriki. ‘kama utaonekana hufai baada ya kuanza uchapishaji, inakuwa ni
vigumu kuongeza muda wa leseni.’
Mamlaka zimefungia leseni za magazeti mara nyingi kwa miaka iliyopita, kwa
mujibu wa washiriki, taarifa za habari na mashirika yasiyo ya kiserikali. Mifano
halisi ni kama Mawio (ambalo lilifungiwa kwa miaka miwili mwaka 2017), na
Mseto (ambalo lilifungiwa kwa miaka mitatu mwaka 2016). Mwaka 2018,
Mahakama ya Afrika Mashariki ilipindua uamuzi uliofanywa na mamlaka
kufungia leseni ya gazeti la Mseto, kwa madai kwamba zuio hilo lilikuwa
‘halina msingi na ni kichekesho,’ kulingana na makala yaliyoandikwa na shirika
lisilokuwa la kiserikali la Utetezi wa Kisheria kwa Vyombo vya Habari.13 Washiriki
walitabanaisha kwamba mamlaka zimedharau uamuzi huo pamoja na maamuzi
mengine kadhaa ya mahakama ambayo yalizuia kufungia vyombo vya habari.

Alama:
Alama za mshiriki mmoja mmoja:
1

Nchi inakidhi kiashiria

2

Nchi inakidhi vipengele vichache tu vya kiashiria

3

Nchi inakidhi vipengele kadhaa vya kiashiria

4

Nchi inakidhi vipengele vingi vya kiashiria

5

Nchi inakidhi vipengele vyote vya kiashiria

Wastani wa alama:
Alama ya miaka iliyopita:

✓✓

✓✓

✓✓

✓

1.6
2006: n/a; 2008: n/a; 2010: 1; 2012: 1.5; 2015: 1.2

12 Sheria ya Vyombo vya Habari ya mwaka 2016 Kifungu cha 8 na cha 9.
13 www.mediadefence.org/news/east-african-court-overturns-tanzania’s-newspaper-ban.

20

✓✓

✓✓✓

KIPIMO CHA VYOMBO VYA HABARI BARANI AFRIKA TANZANIA 2019

Select target paragraph3