ENEO LA 1 za nchi ‘kidogo kidogo’. Washiriki walikuwa pia na mtazamo kwamba mamlaka zilionekana zaidi kutoitambua kabisa mikataba ya kimataifa, ambayo pia inashindwa kuiheshimu. Mathalan, Tanzania haijatimiza wajibu wake wa kutoa taarifa ya mara kwa mara kuhusu hali ya uhuru wa waandishi wa habari na haki za binadamu kwa Umoja wa Afrika na Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za Watu wenye Ulemavu, ambayo inazitaka nchi wanachama kutoa taarifa kuhusu mambo hayo. Kwa kumalizia, mmoja wa washiriki alisema, ‘dhamira yetu kwa viwango vya kimataifa vya haki za binadamu, hata kwenye mahakama, ni ndogo sana kiasi kwamba hata huwa hatuna tabia ya kusema hilo.’ Kumekuwepo na jitihada za kupima hali ya pande mbili za Tanzania na tabia yake ya kutoitambua mikataba ya kimataifa kwa ujumla wake. Mnamo mwaka 2019, Mahakama ya Afrika Mashariki(EACJ) ilitoa uamuzi kwamba vipengele vingi vya Sheria ya Vyombo vya Habari vilikuwa kinyume na uhuru wa kujieleza na uhuru wa wanahabari kama ilivyoelezwa kwenye Mkataba ulioanzisha Jumuiya ya Afrika Mashariki. Mahakama ya Afrika ya Mashariki iliitaka Tanzania kufuta vipengele hivyo, hasa vile vinavyohusu uchochezi, udhalilishaji na utoaji wa taarifa za uongo. Umoja wa Uhuru wa Vyombo vya Habari uliipongeza hukumu hiyo11 kama hatua muhimu katika kupigania uhuru wa kujieleza na uhuru wa vyombo vya habari Tanzania ambao unaendelea kuzorota. Tanzania imekata rufaa dhidi ya hukumu hiyo na wakati AMB ikiendelea, vipengele kandamizi vya Sheria ya Vyombo vya Habari vilikuwa bado vinatumika. Alama: Alama za mshiriki mmoja mmoja: 1 Nchi inakidhi kiashiria 2 Nchi inakidhi vipengele vichache tu vya kiashiria 3 Nchi inakidhi vipengele kadhaa vya kiashiria 4 Nchi inakidhi vipengele vingi vya kiashiria 5 Nchi inakidhi vipengele vyote vya kiashiria Wastani wa alama: Alama ya miaka iliyopita: ✓ ✓ ✓✓✓✓✓✓ ✓ ✓✓ ✓ 2 .1 2006: n/a; 2008: n/a; 2010: 2.2; 2012: 3.3; 2015: 2.5 1.5 Machapisho hayahitaji kupata kibali cha kuchapisha kutoka kwa mamlaka husika Nchini Tanzania, ni kinyume cha sheria kuchapisha gazeti na vyanzo vingine vya habari kwa maandishi bila kupata kwanza leseni kutoka serikalini. Hitaji hili la leseni linahusu kuuza, kusambaza, kuingiza na kutoa habari kwa maandishi popote nchini. Sheria hii inampa mamlaka Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Habari au mwakilishi wake kukataa maombi ambayo hayakidhi matakwa ya leseni na pia kufungia au kufuta leseni ‘endapo mwenye leseni anashindwa kuzingatia 11 Angalia kwa mfano CPJ. Inapatikana mtandaoni kwa anuani: https://cpj.org/2019/03/east-african-court-rules-thattanzanias-media-serv.php. 19 KIPIMO CHA VYOMBO VYA HABARI BARANI AFRIKA TANZANIA 2019