ENEO LA 1 uhuru wa vyombo vya habari. Washiriki walitoa mfano wa Sheria ya Magereza, Sheria ya Makosa ya Kimtandao, Sheria ya Usalama wa Taifa, Sheria ya Maeneo na Sehemu Zilizozuiliwa, Sheria ya Watu Wasiokubalika na hata Sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari kama miongoni mwa sheria kandamizi zaidi na zenye kutumiwa mara nyingi. Sheria ya Maeneo na Sehemu Zilizozuiliwa, kama ilivyo Sheria ya Watu Wasiokubalika, iko nje kabisa ya mipaka ambayo inaweza kuwa na tafsiri anuai na zinazoweza kukiukwa kwa urahisi. Sheria hii inazuia matumizi ya umma ya taarifa zinazopatikana kwenye sehemu zilizoainishwa kwamba zimezuiliwa (kwa mtizamo wa waziri mwenye dhamana), bila kujali kwamba ina maslahi halali ya umma na ya kiusalama). Mmoja wa wanajopo alisema kwamba umma haukujulishwa kuhusu orodha ya maeneo na sehemu ambazo zimezuiliwa, lakini bado wakiukaji wanakabiliwa na hatari ya kifungo cha miaka 20 gerezani endapo watatiwa hatiani. Washiriki walibainisha kwamba kwa kadri itakavyokuwa na mashiko ya kisheria, serikali ina kawaida ya kufukua sheria zilizokwishakusahaulika zamani na kuzitumia. ‘Hatuzungumzii tena sheria hizi kandamizi kwa vile hatutaki kuwakumbusha uwepo wake.’ Alama: Alama za mshiriki mmoja mmoja: 1 Nchi inakidhi kiashiria 2 Nchi inakidhi vipengele vichache tu vya kiashiria 3 Nchi inakidhi vipengele kadhaa vya kiashiria 4 Nchi inakidhi vipengele vingi vya kiashiria 5 Nchi inakidhi vipengele vyote vya kiashiria Wastani wa alama: Alama ya miaka iliyopita: ✓ ✓ ✓ ✓ ✓✓✓ ✓ ✓ ✓ ✓ ✓ 1.8 2006: n/a; 2008: n/a; 2010: n/a; 2012: n/a; 2015: 1.8 1.4 Serikali inaheshimu mikataba ya kikanda na ile ya kimataifa kuhusu uhuru wa kujieleza na uhuru wa vyombo vya habari Tanzania ni nchi ya pande mbili – ni istilahi ya kitaalam inayotumiwa na sheria ya kimataifa kuelezea nchi ambayo inazitenga sheria zake za ndani na mikataba ya kimataifa na mikataba mingineyo. Matokeo yake, mikataba ya kimataifa inayoridhiwa na Tanzania haichukuliwi kama sheria moja kwa moja. Endapo mikataba hiyo haijapata ‘tafsiri’ ya sheria za kitaifa, haitambuliki kama sheria ndani ya Tanzania. Wanajopo walisema kwamba kwa sababu ya utaratibu huu, mikataba ya kimataifa inayohusu uhuru wa kujieleza ambao imeridhiwa na Tanzania ni vigumu kuheshimiwa nchini. Washiriki walieleza kwamba, pale serikali inapoona mikataba ya kimataifa inafaa kwa maslahi yake, basi vifungu vya mikataba hiyo hujumuishwa kwenye sheria 18 KIPIMO CHA VYOMBO VYA HABARI BARANI AFRIKA TANZANIA 2019