ENEO LA 1 Kwa kuwa fursa ya kujieleza kwa uhuru inafungwa, watanzania wengi wanatoa mawazo ya mitandaoni. Hata hivyo, washiriki wanasema, wananchi wanaona haja ya kutumia majina bandia. Kwa vile hofu imetanda kwenye majukwaa ya mtandaoni, washiriki walisema kwamba wana wasiwasi kwamba mtindo wa wanachi binafsi na hata mamlaka kutumia vifaa vinavyojiendesha vyenyewe kama vile kompyuta kutoa maoni mmoja ili kuficha utambulisho wao, kwa upande mmoja, na kwa upande mwingine kuweza kupata utambulisho wa watumiaji wa mitandao. Hata hivyo, siyo kila mmoja anahofia kusema anachotaka kwa njia tofauti ambayo inaweza kumchanganya mgeni- ambayo mshiriki mmoja aliielezea kwamba inatokana na utamaduni ‘uliopo wa viwango tofauti’. Vyanzo vichache vya habari, kama vile gazeti la Tanzanite, vimebakia gumzo kwa kiasi kikubwa. Kwa kuangalia kile wanachoweza kukiandika na kukikana, mtu anaweza kudhani kwamba kuna uhuru wa kujieleza Tanzania’, alisema mmoja wa washiriki. Washiriki walidai kwamba vyombo hivi vinaendeshwa na kuwezeshwa na watu wanaoipendelea serikali na hivyo havina madhara kwa utawala. Kwa ufupi, sheria kandamizi za vyombo vya habari kwa kiasi kikubwa zimeathiri matumizi ya haki ya uhuru wa kujieleza Tanzania kwa waandishi wa habari na wananchi halikadhalika. Hali hii imekuwa na athari hasi kwenye weledi wa waandishi wa habari na wanazuoni wengine kama vile watafiti na watetezi wa haki za binadamu kufanya kazi zao, lakini pia ubora wa uhandishi wa habari na mawasiliano mengine. Katika mazingira yaliyopo, washiriki walihisi kwamba ilikuwa vigumu kutegemea kwamba wananchi, wakiwemo waandishi wa habari, wanatumia haki zao za uhuru wa kujieleza pasi na hofu. Alama: Alama za mshiriki mmoja mmoja: 1 Nchi inakidhi kiashiria 2 Nchi inakidhi vipengele vichache tu vya kiashiria 3 Nchi inakidhi vipengele kadhaa vya kiashiria 4 Nchi inakidhi vipengele vingi vya kiashiria 5 Nchi inakidhi vipengele vyote vya kiashiria Wastani wa alama: Alama ya miaka iliyopita: ✓✓ ✓ ✓✓ ✓ ✓ ✓ ✓ ✓ ✓✓ 2.0 2006: 2.1; 2008: 2.8; 2010: 2; 2012: 3.3; 2015: 2.7 1.3 HAKUNA vigingi vya kisheria kwa uhuru wa kujieleza au sheria zinazoingilia utendaji wa vyombo vya habari (mathalan, siri za kiofisi, ukosoaji na matakwa ya kisheria) Kwa takwimu za hivi karibuni, Tanzania ilikuwa na vifungu vya sheria takriban 24 ambavyo vinaweza kutumiwa kukanyaga haki za raia za uhuru wa kujieleza na 17 KIPIMO CHA VYOMBO VYA HABARI BARANI AFRIKA TANZANIA 2019