ENEO LA 1 ambavyo vitarusha mikutano inayofanywa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu.9 Mwaka 2019, taarifa yenye kichwa cha habari Yearbook on Media Quality in Tanzania 2018: Synthesised Report on Overall Results (Taarifa ya Mwaka kuhusu Ubora wa Vyombo vya Habari Tanzania 2018: Taarifa Iliyotolewa kuhusu Matokeo ya Jumla) ilionesha kwamba habari za kisiasa kwenye vyombo vya habari vya Tanzania zilikuwa zimeshuka kwa kwa kiwango kikubwa.10 Washiriki waliongezea kwa kusema kwamba taarifa za habari zilikuwa ‘zinatoka kwenye chanzo kimoja kwa kuwa inazidi kuwa vigumu kulinganisha habari au kuwa na taarifa kuhusu vyanzo’. Kwa mujibu wa mawasilisho yao, hata mawaziri na maafisa wa ngazi za juu wa serikali wamekuwa wakikataa kuongea na waandishi wa habari. Washiriki walisema kwamba kwa mazingira haya, habari, uchambuzi na makala yenye kukosoa serikali vyote vimetoweka kwenye magazeti. Pale ambapo bado vipo, ‘lugha ya uwasilishaji imebadilika’, alisema mmoja wa washiriki. ‘Unajua inabidi usome mistari mitatu ya chini ili uweze kuelewa kinachozungumzwa.’ Wanajopo walisema kwamba nje ya vyombo vya habari na waandishi wa habari, wananchi hawawezi kutoa mawazo yao kwa uhuru. ‘Redio mbao’ ni msemo unaoelezea njia za mawasiliano yasiyo rasmi kama vile mazungumzo ya mitaani ambayo yalikuwa yamekidhiri kwenye mitaa ya Kiafrika, navyo viko kimya. ‘Zamani, watu waliongea habari za siasa wazi wazi nje ya vituo vya kuuzia magazeti au kwenye vituo vya mabasi. Lakini siku hizi, mada imebadilika na kuwa soka au dini”. Baadhi ya wanajopo walisema kwamba hata mijadala kwenye mitandao ya kijamii ilikuwa imedhibitiwa vilivyo, hasa kwa kutumia sheria mpya ambazo zinawawajibisha waendeshaji wa mijadala kwenye mitandao ya kijamii hata kwa habari iliyotumwa na mchangiaji wa kawaida. Baadhi ya washiriki walisema kwamba ilikuwa imekuwa ni kawaida kutolewa kwenye kundi la WhatsApp au Facebook kwa sababu ya kutoa maoni yanayoonekana kuwa na mguso, ‘watu wamegundua kwamba kuna uhuru wa kujieleza lakini hakuna uhuru baada ya kujieleza. [Kutumia haki ya] uhuru wa kujieleza kunategemea unachokisema na ni nani unayemzungumzia.’ Vifungu vya zamani vya adhabu dhidi ya ‘wahuni na wazururaji’, ambavyo vinaharamisha uzururaji na kukaa bila kazi vimechimbuliwa hivi karibuni na vimeongezewa mkazo. Washiriki walisema hali kama hiyo imeonekana kwenye matumizi ya Sheria ya Watu Wasiokubalika, sheria ya chinichini iliyobakia tangu wakati wa utawala kandamizi wa kiloni. Katika mfano mmoja uliotolewa na mwanajopo anayejua mkasa huo, wanafunzi wa chuo kikuu kimoja cha Tanzania walikamatwa na kushtakiwa kwa uzuraji mwaka 2018, baada ya polisi kuwakuta wakijadili mambo ya kisiasa. Washiriki walisema kwamba mamlaka zilikuwa zikitumia sheria hizi za zamani lakini ambazo bado hazijafutwa ili kuwazuia vijana ‘kukaa vijiweni’ na uwezekano wa wao kujadili mambo ya kisiasa. 9 Shirika la Kutetea Haki za Binadamu (HRW) lilisema hayo kwenye mkutano na waandishi wa habari, LHRC ilijadili tuhuma za serikali kuhusu matumizi mabaya ya madaraka wakati wa uchaguzi mkuu wa Rais mwaka 2017. Vyombo vya habari vilivyopigwa faini vilishtakiwa kwa kutangaza habari za kichochezi na kukiuka Sheria ya Utangazaji. https://www.hrw.org/ world-report/2019/country-chapters/tanzania-and-zanzibar. mara ya mwisho ilipatikana tarehe 20 Mei 2019. 10 Spurk, C &Katunzi, A. 2019. Yearbook on Media Quality in Tanzania 2018: Synthesised Report on Overall Results. Media Council on Tanzania and Spurk Media Consulting Ltd. 16 KIPIMO CHA VYOMBO VYA HABARI BARANI AFRIKA TANZANIA 2019