ENEO LA 1 yamekosolewa na watu na taasisi mbalimbali kwamba ni kinyume na sheria5 lakini bado yameendelea kutumika. Mwezi Machi 2019, pamoja na sababu nyinginezo, sheria hii ilitumika kufungia kwa muda gazeti la The Citizen kwa kuandika habari bila kibali kuhusu viwango vya ubadilishaji fedha za kitanzania dhidi ya Dola ya Kimarekani.6 Mamlaka zilisema kwamba gazeti hilo lilifungiwa kwa kurudia kutoa taarifa za uongo na za kichochezi. Hata hivyo, mmoja wa wanajopo alisema, ‘Taarifa hizo zilikuwa za kweli. Tatizo ni kwamba uthibitisho wa taarifa hizo haukufanywa na NBS’. Kwa mujibu wa wanajopo, hujuma dhidi ya uhuru wa habari na uandishi wa habari unaanzia kwenye matumizi mabaya ya sheria hadi mashambulizi ya ana kwa ana ya kimwili. Kati ya mwaka 2016 na 2017, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), ambacho ni taasisi isiyo ya kiserikali, kiliorodhesha matukio 17 ya unyanyasaji dhidi ya waandishi wa habari na watetezi wa haki za binadamu na matukio mengine mengi dhidi ya raia wengine.7 Mwandishi wa habari za kiuchunguzi Azory Gwanda alitoweka mwezi Novemba 2017, na hadi wakati wa kuchapisha taarifa hii hakuna taarifa yoyote kama bado yuko hai. Asasi za kiraia wanakosoa kutokufanyika kwa uchunguzi wa tukio hili. Kwa mujibu wa wanajopo na Article 19 Eastern Africa, Gwanda alikuwa akichunguza matukio ya mauaji yaliyolenga viongozi wa kimaeneo na maafisa usalama, baadhi ya matukio hayo yakidaiwa kufanywa na ‘washambuliaji wapanda pikipiki wasiojulikana’, wakati alipochukuliwa na watu wasiojulikana asubuhi ya tarehe 21 Novemba 2017.8 Utata unaoonekana wa serikali dhidi ya uhuru wa kujieleza umeibua woga. Wanajopo walibainisha kwamba waandishi wa habari na taasisi za vyombo vya habari wamelazimika kujichuja wenyewe na hivyo kuwa waangalifu na kuchagua habari za kuandika kwa sababu hatari ya kuadhibiwa imekuwa kubwa. Mmoja wa washiriki alielezea mazingira ya sasa kama ifuatavyo: Waandishi wa habari watakuambia kwamba hawako huru. Sasa hivi, kama unataka kupata mafanikio katika uandishi wa habari, ni lazima uimbe nyimbo za kuitukuza serikali au uandike habari zile tu ambazo wale walioko madarakani wanataka kuzisikia. Uandishi wa habari za kiuchunguzi hazina mpango tena Tanzania. Hata kutoa taarifa za matukio kwa sasa ni hatari sana. Kwa mfano, mamlaka ziliweka adhabu ya shilingi milioni 60 (Dola za Kimarekani 27,000) kwa vituo vya luninga 5 6 7 8 Angalia: Benki ya Dunia (2018). Taarifa ya Benki ya Dunia kuhusu Marekebisho ya Sheria ya Takwimu ya Tanzania ya mwaka 2015. Inapatikana mtandaoni kwa anuani hii: https://www.worldbank.org/en/news/statement/2018/10/02/worldbank-statement-on-amendments-to-tanzanias-2015-statistics-act. Mara ya mwisho ilipatikana tarehe 20 Mei 2019. Angalia gazeti la Daily Monitor (linapatikana mtandaoni kwa anuaani hii: https://www.monitor.co.ug/News/National/ Tanzania-bans-Citizen-newspaper/688334-5002850-r04jl4z/index.html) na CPJ (Inapatikana mtandaoni kwa anuani hii: https://cpj.org/2019/03/tanzania-citizen-7-day-publication-ban.php) Taarifa zote mbili zilipatikana tarehe 20 Mei 2019. FIDH and LHRC (2017). Tanzania: Uhuru wa Kujieleza Mashakani, Joint Situation Note. No 698a. Inapatikana mtandaoni kwa anuani hii:: https://www.fidh.org/IMG/pdf/joint_position_note_tanzania_fidh_lhrc.pdf. Mara ya mwisho ilipatikana tarehe 21 Mei 2019. Angalia Article 19 East Africa. Linapatikana mtandaoni kwa anuani: https://www.article19.org/resources/tanzaniaconcern-grows-missing-journalist-azory-gwanda/. Mara ya mwisho kupatikana ilikuwa tarehe 20 Mei 2019. 15 KIPIMO CHA VYOMBO VYA HABARI BARANI AFRIKA TANZANIA 2019