ENEO LA 1 ambayo ingekuwa na mabadiliko chanya, ambayo inatoa uhuru kwa vyombo vya habari, imefungiwa ndani na hivyo kufifisha matumaini kuleta mabadiliko kwenye hali ya vyombo vya habari wakati wowote kwa siku za karibuni. Alama: Alama za mshiriki mmoja mmoja: 1 Nchi inakidhi kiashiria 2 Nchi inakidhi vipengele vichache tu vya kiashiria 3 Nchi inakidhi vipengele kadhaa vya kiashiria 4 Nchi inakidhi vipengele vingi vya kiashiria 5 Nchi inakidhi vipengele vyote vya kiashiria Wastani wa alama: Alama ya miaka iliyopita: ✓ ✓✓ ✓ ✓✓✓✓✓✓✓ ✓ 2.3 2006: 2.8; 2008: 2.4; 2010: 2.7; 2012: 2.5; 2015: 2.7 1.2 Haki ya uhuru wa kujieleza inatumiwa na wananchi, wakiwemo waandishi wa habari, bila hofu Mwaka 2017, Tanzania iliyafungia magazeti manne kwa muda, na hiki kilikuwa kitendo cha aina yake kufanyika ndani ya mwaka mmoja katika historia ya hivi karibuni ya Tanzania. Hatua hii iliongeza idadi ya machapisho yaliyofungiwa kufikia matano katika kipindi cha miaka miwili na ilidhihirisha mwendelezo wa mazingira mabaya na yenye changamoto kwa tasnia ya uhandishi wa habari na uendeshaji wa vyombo vya habari. Hatua hiyo ilifuatiwa na maonyo na kukumbushia kulikofanywa na Rais kwamba upashaji habari Tanzania unapaswa kuzingatia maadili. Mwezi Oktoba mwaka 2017, Bwana Henry Maina, Mkurugenzi wa Kanda wa Article 19 Eastern Africa, shirika lisilo la kiserikali lenye kujishughulisha na haki za vyombo vya habari, alisema kwamba, ‘Kufungiwa kwa magazeti ni hujuma dhidi ya uhuru wa vyombo vya habari nchini na kunadhoofisha wajibu wa vyombo vya habari kama waangalizi katika jamii ya kidemokrasia. Ni habari mbaya kwamba Tanzania inaonekana kurudi nyuma katika dhamira yake ya kutoa uhuru kwa vyombo vya habari kwa kufungia taasisi za habari bila sababu za msingi. Kufungia vyombo vya habari kama hivi kunaweza pia kusababisha waandishi wa habari kujihariri wenyewe na hivyo kuchagua habari.’4 Wanajopo walisema kwamba serikali imetumia sheria kandamizi na mamlaka yake makubwa kukanyaga uhuru wa kujieleza. Moja kati ya silaha ya hatari kabisa zilizo kwenye mikono ya mamlaka ni sheria mpya ambayo inazuia matumizi ya takwimu rasmi bila idhini. Marekebisho ya mwaka 2018 ya Sheria ya Taifa ya Takwimu ya mwaka 2015 inataka idhini ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kabla ya kuchapisha takwimu rasmi; serikali ilidai kwamba marekebisho haya yalihitajika ili kulinda ukweli na uhalisi wa takwimu. Marekebisho haya 4 14 https://www.article19.org/resources/tanzania-ban-on-newspapers-raises-concerns-for-press-freedom/. KIPIMO CHA VYOMBO VYA HABARI BARANI AFRIKA TANZANIA 2019