ENEO LA 1 mahakama yoyote ya masuala ya madai au ya jinai; kulinda heshima, haki na uhuru wa watu wengine au usiri wa watu wanaohusika katika mashauri mahakamani, kuzuia utoaji wa taarifa za siri, au kulinda heshima, mamlaka na uhuru wa mahakama; kuzuia uundwaji, usimamizi na shughuli za taasisi na mashirika binafsi nchini; au kitu kingine chochote kitakachofanyika kwa ajili ya kuendeleza au kuhifadhi maslahi ya taifa kwa ujumla. Kinyume na kanuni inayokubalika kwa ujumla ambayo inachukulia katiba kama sheria mama, wanajopo walisema kwamba inapofika suala la haki na uhuru, Katiba ya Tanzania inapwaya. Walirudia na kunukuu Kifungu cha 30(5) cha Katiba hiyo, ambapo walisema kwamba ni vigumu kudai haki na uhuru wa kikatiba kwa kuwa inawapa majaji mamlaka kuvuka mipaka ya kikatiba panapokuwepo mgongano wa kimaslahi. Kifungu hicho kinaeleza kwamba: Katika shauri lolote, inapodaiwa kwamba sheria yoyote iliyotungwa au hatua yoyote itakayochukuliwa na serikali au mamlaka nyingine yoyote inavunja au kuminya haki yoyote ya msingi, uhuru na wajibu kama ilivyoelezwa kwenye vifungu vya 12 hadi 29 vya Katiba hii, na Mahakama Kuu ikajiridhisha kwamba sheria au kitendo husika, kwa kadri kwamba inakinzana na Katiba hii, ni batili, au ni kinyume na Katiba hii, Mahakama Kuu, kama ikiona hivyo, au kama mazingira au maslahi ya umma yanahitaji hivyo, badala ya kuamua kwamba sheria hiyo au kitendo hicho ni batili, itakuwa na mamlaka ya kuamua kuipa serikali au mamlaka nyingine inayohusika muda wa kurekebisha kasoro zilizobainishwa kwenye sheria au kitendo husika kwa muda na namna ambavyo Mahakama Kuu itaamua, na sheria hiyo au kitendo hicho kitahesabika kuwa halali hadi pale kasoro hizo zitakapokuwa zimerekebishwa au muda utakaowekwa na Mahakama Kuu utakapokuwa umemalizika, kutegemeana na kipi kinatangulia. Pamoja na mianya iliyopo kwenye Katiba, wanajopo waliona kwamba vipengele mbalimbali vya sheria vimepitishwa na mara nyingi vinasimamiwa ambavyo vinakiuka vifungu vya Katiba ambavyo vinatoa uhuru wa kujieleza. Baadhi ya sheria mbaya kabisa ni pamoja na Sheria ya Makosa ya Mtandaoni na Sheria ya Magereza. Baadhi ya sheria hizi zimeibuka hivi karibuni kabisa na mifano mizuri ni Sheria ya Vyombo vya Habari ya Mwaka 2016, ambayo kwa mara nyingine imeingiza makosa ya uchochezi na kutoa kashfa, ikiwemo kuwakashfu marehemu. Wanajopo walisema kwamba kiujumla, kuna dalili za kutungwa kwa sheria kandamizi zaidi ambazo zinaweka vigingi kwa watu na taasisi kutumia haki yao ya uhuru wa kujieleza na uhuru wa vyombo vya habari. Wakitolea mfano Sheria ya Vyombo vya Habari, mmoja wa washiriki alisema, “Sheria ya Magazeti ya Mwaka 1976, ambayo ilionekana kuwa kandamizi, ilirithiwa na sheria kandamizi zaidi, yaani Sheria ya Vyombo vya Habari. Tuliomba mkate na badala yake tukapewa nyoka.” Kwa muhtasari, washiriki walionesha kwamba pamoja na kwamba Katiba inatambua uhuru wa kujieleza kama haki, inashindwa kuilinda haki hizo, haizungmzii uhuru wa vyombo vya habari na imeacha mianya inayoruhusu kushamiri kwa sheria nyingine ambazo zinaweza kukiuka haki hizo. Katiba 13 KIPIMO CHA VYOMBO VYA HABARI BARANI AFRIKA TANZANIA 2019