ENEO LA 1 (1) Kila mtu ana haki na uhuru wa (a) kutafuta, kupata, na kutoa habari na taarifa; na (b) kuanzisha chombo cha habari na njia nyinginezo za kusambaza habari bila kujali mipaka ya kitaifa. (2) Vyombo vya habari vitakuwa huru na vitakuwa na (a) haki ya kupata, kutumia na kutoa habari na taarifa wanazopata; (b) jukumu la (i) kutoa habari na taarifa kwa umma; na (ii) kuheshimu na kulinda utu, heshima, uhuru na hadhi ya raia dhidi ya habari na taarifa wanazopokea, kuandaa na kusambaza. (3) Serikali na taasisi zake, asasi za kiraia na watu binafsi watawajibika kwa kutoa taarifa kwa umma kuhusu shughuli na utekelezaji wa shughuli zao. (4) Bunge litatunga sheria kwa minajili ya kulinda: (a) haki na uhuru wa vyombo vya habari; na (b) habari na taarifa kwa minajili ya usalama wa taifa, amani, maadili ya umma, haki, heshima na uhuru wa watu wengine. Pamoja na mtizamo wake chanya, wanajopo wamebaini kwamba uhuru wa vyombo vya habari uliopendekezwa kwenye katiba mpya haukuwa na tija kama katiba mpya itaendelea kufungiwa kwenye makabati- kama hali ilivyokuwa wakati wa kufanya tathmini hii ya hali ya vyombo vya habari kwa Tanzania. Aidha, wanajopo walikuwa na mtizamo usioridhisha kwa ujumla kuhusu kiasi ambacho katiba iliyopo inatoa uhuru wa kujieleza na uhuru wa vyombo vya habari: Kueleza [uhuru wa kujieleza] kwenye katiba ni kitu kimoja, kutoa uhuru huo ni kitu kingine. Kutoa ina maana kwamba hatua zinachukuliwa kuhakikisha kwamba raia wanapata haki hizo. Lakini hali ni tofauti. Kusema kweli, hakuna haki yoyote inayotolewa katika nchi ya Tanzania. [Badala yake] sheria zinazotakiwa kuchagiza haki hizi zimetengenezwa kwa mtindo wa kuzidhoofisha haki hizo. Katiba yenyewe pia imeweka mipaka katika kutumia haki hizo na uhuru huo, ikizingatiwa kwamba kifungu cha 30 kinaeleza kwamba haki zinatumiwa pale tu zinapokuwa hazikiuki haki za watu wengine na maslahi mapana. Na kwa kukazia zaidi, kifungu hicho kinaongezea kwamba vifungu vya katiba vinavyoainisha haki za msingi za binadamu, uhuru na wajibu haviizuii serikali kusimamia sheria zilizopo au kutunga sheria nyingine ambazo zinaweza kuathiri haki na uhuru wa raia ulioainishwa kwenye katiba. Kwa mfano, katiba inabainisha kwamba haki, uhuru na wajibu wa raia vinaweza kuingiliwa kwa madhumuni ya: Kuhakikisha kwamba haki na uhuru wa watu wengine au maslahi ya umma hayazuiliwi na matumizi mabaya ya uhuru na haki za watu binafsi; Kuhakikisha kwamba ulinzi, usalama wa umma, utulivu wa umma, maadili ya umma, afya ya jamii, mipango ya mijini na vijijini, uchimbaji na matumizi ya madini au kuongeza na kuendeleza mali au maslahi mengine yoyote kwa ajili ya kuimarisha maslahi ya umma; kuhakikisha utoaji maamuzi au amri ya mahakama inayofanya au kutolewa katika 12 KIPIMO CHA VYOMBO VYA HABARI BARANI AFRIKA TANZANIA 2019