ENEO LA 1 1.1 Uhuru wa kujieleza, ukiwemo uhuru wa vyombo vya habari, umeainishwa kwenye katiba na unapewa msukumo na vipengele vingine vya sheria Kama ilivyo kwa nchi nyingi za kileo, Tanzania inaongozwa kwa mujibu wa katiba, ambayo kimsingi, ndiyo sheria mama. Mnamo mwaka 2011, Tanzania ilianzisha mchakato wa kutunga katiba mpya ambayo ingekuwa na ‘uhalali na maridhiano ya kitaifa zaidi’. Rasimu ya katiba hiyo ilikuwa na mabadiliko makubwa sana kuhusiana na mkataba kati ya umma na viongozi wa serikali: lakini ilipingwa kwa nguvu zote. Vyama vya upinzani na asasi za kiraia zililalamika kwamba, Bunge la Katiba Tanzania halikuwa na uwakilishi sawia na rasimu waliotengeneza haikuzingatia maoni ya upinzani kama vile vipengele vinavyopunguza madaraka ya Rais. Yaliyojiri baadae na kusababisha mchakato huo kusimama ni kwamba tume ya uchaguzi ilisitisha kura ya maoni iliyokuwa imepangwa kwa ajili ya Katiba mpya ya Mwaka 2015, na kusema rasmi kwamba uandikishaji wa daftari la wapiga kura ulikuwa umechelewa. Wanajopo wa AMB walisema kwamba kurejesha mchakato wa katiba mpya hakuonekani kama kipaumbele cha serikali iliyopo madarakani, ambayo iliingia madarani kwa kupitia uchaguzi uliofanyika baadae mwaka 2015. Kwa hivyo, Katiba ya Mwaka 19773 bado ilikuwa na nguvu kisheria wakati wa tathmini ya mwaka 2019 ya hali ya vyombo vya habari Tanzania. Katiba hii inatambua haki na wajibu kadha wa kadha wa raia, ikiwamo haki ya kujieleza. Haki hii imejumuishwa chini ya vifungu kadhaa vinavyohusiana na ‘haki ya uhuru wa utambuzi.’ Kifungu cha 18 cha Katiba ya Tanzania ya Mwaka 1997 kinaeleza kuwa: Kila mtu (a) ana haki ya kutoa maoni na kueleza mawazo yake; (b) ana haki ya kutafuta, kupata na/au kutoa taarifa bila kujali mipaka ya kitaifa; (c) ana uhuru wa kuwasiliana na uhuru wa kulindwa dhidi ya kuingiliwa mawasiliano yake; na (d) ana haki ya kupewa habari wakati wote kuhusu matukio mbalimbali muhimu ya kimaisha na shughuli za watu na pia kuhusu masuala muhimu kwenye jamii. Ni dhahiri kwamba Katiba hii imeshindwa kuwa wazi kuhusu suala la uhuru wa vyombo vya habari. Wanajopo walibaini kwamba baadhi ya sheria zilizotumika wakati wa ukoloni bado zinatumika ambapo inajulikana kwamba kiasilia sheria hizo ni kandamizi. Shukrani ziwaendee mashirika ya haki za vyombo vya habari kwa kuwa mswada mpya wa katiba mpya ulijumuisha vipengele mahsusi vinavyohusu ‘uhuru wa kupata habari na uhuru wa vyombo vya habari’. Kifungu cha 31 cha katiba mpya kinaeleza kwamba: 3 Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 imeshafanyiwa marekebisho mara 14s. Marekebisho ya mwisho yalifanyika mwaka 2005. Angalia Utangulizi wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 11 KIPIMO CHA VYOMBO VYA HABARI BARANI AFRIKA TANZANIA 2019