Ingawa huduma za matangazo (hasa kwa njia ya redio) zinapatikana kwenye sehemu kubwa ya nchi, kuna mawanda finyu sana kwenye vyombo vya habari. Tanzania ni jamii mchanganyiko yenye makabila zaidi ya 120 pamoja na lugha za kijamii, lakini mchanganyiko huu haujidhihirishi kwenye vyombo vya habari kwa sababu sheria inazuia matumizi ya lugha za kijamii kwenye vyombo vya habari. Shirika la utangazaji la taifa -Shirila la Utangazaji Tanzania (TBC), ambalo linatakiwa kuwafikia watu wote, linadhibitiwa vikali na hutumiwa kama kipaza sauti cha serikali au chama tawala, na hivyo kuzima sauti za watu wenye mawazo mbadala. Sauti za wanawake mara nyingi huzimwa kwenye vyombo vya habari. Kwa mujibu wa mtandao wa GenderLinks, wanaume bado wanatawala kwenye vyombo vya habari Tanzania.1 Wanawake wanaofanya kazi kwenye vyombo vya habari pia hunyanyaswa kijinsia. Utafiti uliofanywa na Internews kuhusu mchango wa wanawake kwenye vyombo vya habari ulionesha kukithiri kwa unyanyasaji wa kijinsia kwenye taasisi zote za habari.2 Wanawake pia wanazungumziwa vibaya na viongozi wa serikali na vyombo vya habari. Mazingira ya vyombo vya habari na waandishi wa habari yamedorora kwa kiasi kikubwa katika miaka ya karibuni; na kwa uchache, magazeti manne yamefungiwa tangu mwaka 2017. Sheria kandamizi, matumizi ya adhabu kubwa na kukamatwa bila kushtakiwa ni baadhi ya mambo yanayowakuta waandishi wa habari. Vilevile, mwanahabari Azory Gwanda ametoweka nyumbani tangu mwezi Novemba 2017. Kabla ya kutoweka, alikuwa ameandika makala kadhaa yaliyoelezea mauaji ya viongozi wengi wa kimaeneo na maofisa wa polisi. Kutoweka kwake kumesababisha hali ya sintofahamu kwa vyombo vya habari. Waandishi wa habari na vyombo vya habari wamelazimishwa kujihariri wenyewe. Hali ya sintofahamu haipo tu kwa vyombo vya habari lakini pia inawapata hata wanajamii. Watu wanaogopa kubadilishana mawazo ya kisiasa kwa uhuru na angalizo hili limeingia pia kwenye mijadala mitandaoni. Changamoto nyingine kama vile kushuka kwa viwango vya utoaji taarifa, na rushwa kwa ujumla wake pia zinavikabili vyombo vya habari. Kwa mfano, haki na usahihi katika utoaji habari vinazidi kuporomoka kutokana na sababu anuai kama vile mafunzo hafifu, uharakishaji unatokana na hitaji la kwenda na muda na kuondoka kwa wanahabari nguli. Mbaya zaidi, waandishi wa habari wa Tanzania hawalipwi vizuri. Waandishi wengi hawana mikataba ya ajira, na kwa hivyo, hawapati mafao wanayostahili. Kwa kukosa umoja katika kushughulikia kero zao, waandishi wengi hujihusisha na rushwa. Uhandishi wa habari wa bahasha ya kahawia, ambapo waandishi wa habari hupewa bakhshishi ya fedha ili kuandika habari kwa upendeleo au kuzima habari zenye taswira hasi, unazidi kushika kasi nchini. Pamoja na hali ya kusikitisha ya hali ya kisiasa na vyombo vya habari, bado kuna matumaini. Ingawa taasisi za kiraia zimekuwa zikilalamikia kuongezeka kwa 1 2 8 Jambo hili liliibuliwa na Mkurugenzi Mtendaji wa GenderLinks, Colleen Lowe Morna, kwenye Mkutano wa Kilele kuhusu Jinsia na Upashaji Habari kuhusu Maendeleo Endelevu uliofanyika Tanzania mwaka 2018. Taarufa ya Uchambuzi wa Usawa wa Kijinsia na Ushirikishaji wa Kijamii uliofanywa na FHI 360 kwa ushirikiano na Internews. KIPIMO CHA VYOMBO VYA HABARI BARANI AFRIKA TANZANIA 2019