mbinyo wa serikali mwaka mzima kwa njia ya vitisho, uchunguzi, ukamataji na sheria kali, taasisi za kiraia Tanzania (CSOs) na mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) bado vina nguvu. Mara nyingi asasi za kiraia huungana na kuchagiza mapambano dhidi ya sheria ambazo zinaathiri uhuru wa vyombo vya habari. Muungano wa Haki ya Habari umeweza kuunganisha nguvu ya taasisi kadha wa kadha za kiraia kuongoza mapambano ya kimkakati dhidi ya sheria kandamizi za vyombo vya habari. Muungano wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania na Jukwaa la Muungano wa Asasi za Kiraia Afrika Mashariki wanasifika pia kwa kuchukua hatua dhidi ya masahibu ya vyombo vya habari. Mfano wa hivi karibuni ni mapema mwaka 2019 ambapo mashirika matatu yasiyo ya kiserikali Tanzania yalifungua mashtaka dhidi ya Sheria ya Vyombo vya Habari kwenye Mahakama ya Afrika Mashariki (EACJ). Mahakama hiyo iliamua kwamba vipengele anuai vya Sheria ya Vyombo vya Habari vinaminya uhuru wa vyombo vya habari na uhuru wa kujieleza, na hivyo kuitaka serikali ya Tanzania kuifutilia mbali sheria hiyo. Tanzania inaelekea kwenye uchaguzi mkuu mwaka 2020. Tangu ilipohama kutoka kwenye nchi ya chama kimoja cha siasa na kwenda kwenye mfumo wa vyama vingi, Tanzania imekuwa inafanya chaguzi za amani kwa kiasi fulani. Hata hivyo, mgawanyiko wa kisiasa unaozidi kuongezeka hivi sasa unaashiria wasi wasi mkubwa katika chaguzi hizi zinazokuja. Kama ilivyo kwa chaguzi nyinginezo duniani, kuna ongezeko katika matumizi ya wataalam wapotoshaji kwenye mitandao ya kijamii ili kupindisha mawazo na mitizamo huru. Upotoshaji huu unaofanyika kwa njia ya mtandao pamoja na kujitafutia umaarufu wa kisiasa na mabadiliko katika uthibiti unachangia sana kushusha kiwango cha chaguzi huru na za haki ambazo zimeiletea Tanzania sifa kubwa katika ukanda wa Afrika ya Mashariki. Mjadala huu ulifanyika kwenye hoteli ya White Sands, Dar es Salaam, Tanzania Mei 2019. 9 KIPIMO CHA VYOMBO VYA HABARI BARANI AFRIKA TANZANIA 2019