Kwa miaka ya 2009, 2013 na 2019, baadhi ya viashiria vilibadilishwa ili kuakisi mabadiliko katika hali ya vyombo vya habari. Matokeo yake ni kwamba, kwenye baadhi ya maeneo, ulinganishi wa viashiria vya taarifa zilizopita hauendani kwa vile kiashiria ama ni ingizo jipya au kimefanyiwa marekebisho makubwa. Majumuisho ya kipengele kimojakimoja yanagawanywa kwa idadi ya wanajopo ili kukokotoa wastani wa alama kwa kila kiashiria. Wastani wa alama katika kila kiashiria unajumlishwa ili kupata wastani wa alama katika eneo lengwa. Matokeo Taarifa ya mwisho ya kitaamuli inatoa muhtasari wa maelezo ya jumla ya mjadala ambao huonesha wastani wa alama kwa kila kiashiria. Majina ya wanajopo hayatambulishwi kwenye taarifa ili kuwaepusha na madhara yanayoweza kuwapata kutokana na michango yao katika mijadala. Taarifa hizi zinaweza kutumiwa kama nyenzo ya kuibua mjadala wa kisiasa kuhusu marekebisho ya mazingira ya vyombo vya habari. Katika nchi ambazo Kiingereza siyo lugha rasmi, taarifa huchapishwa katika lugha mbili. Ili kuwafanya AMB, FES na MISA kubakia kama wenyeji wa wanajopo na watoaji wa zana za utafiti, yaliyomo katika majadiliano pamoja na taarifa hubakia kuwa mali ya jopo la wataalam wa ndani ya nchi na hayawakilishi au kuakisi maoni ya FES au MISA. Kufikia mwishoni mwa mwaka 2019, AMB ilikuwa imeshakamilika kwa mafanikio mara 121 katika nchi 32 za kiafrika, na katika baadhi ya nchi hizo ikiwa ni kwa mara ya sita tayari. Luckson Chipare Mkurugenzi wa Kanda Taasissi ya Vyombo vya Habari Afrika Kusini (MISA) Windhoek, Namibia 3 Freya Gruenhagen Mkurugenzi fesmedia Africa Friedrich-Ebert-Stiftung Windhoek, Namibia KIPIMO CHA VYOMBO VYA HABARI BARANI AFRIKA TANZANIA 2019