Kipimo cha Vyombo vya Habari Barani Afrika Kipimo cha Vyombo vya Habari Barani Afrika (AMB) ni tathmini yakinifu na kamilifu; na mfumo wa upimaji wa mazingira ya kitaifa ya vyombo vya habari katika bara la Afrika. Tofauti na tafiti nyingine zinazohusu vyombo vya habari au vipimo vya vyombo vya habari, AMB ni tathmini rejeshi yenye kuzingatia vigezo vya ndani ya nchi vinavyotokana na Mikataba na Maazimio ya Afrika kama vile Azimio la Kanuni za Uhuru wa Kujieleza Afrika la mwaka 2002 lililotolewa na Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu na Haki za Watu. Zana za utafiti huu ziliundwa kwa ushirikiano kati ya fesmedia Africa, ambao ni mradi wa vyombo vya habari wa Friedrich-Ebert-Stiftung (FES) barani Afrika, na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) mnamo mwaka 2004. AMB ni uchambuzi unaolenga kupima hali ya vyombo vya habari katika nchi husika na wakati huohuo kuwa kama nyenzo ya kushawishi uboreshaji wa mazingira ya vyombo vya habari. Matokeo ya utafiti hutolewa kwa wananchi wa nchi husika ili waweze kushawishi maboresho ya hali ya vyombo vya habari kwa kuzingatia Maazimio ya Umoja wa Afrika (AU) pamoja na mifumo ya Kiafrika kama vielelezo. Mapendekezo yanayotolewa kwenye taarifa ya AMB hatimaye yanajumuishwa kwenye tathmini nyinginezo zilizofanyika kwenye nchi zipatazo 20 zenye ofisi za FES Kusini mwa Bara la Afrika, na kujumuishwa pia kwenye jitihada mbalimbali za ushawishi kuhusu vyombo vya habari unaofanywa na taasisi nyingine za vyombo vya habari katika nchi husika kama vile MISA. Mbinu na mfumo wa utoaji alama Kila baada ya miaka mitatu hadi minne, jopo la wataalam kati ya 10 na 12 lenye kujumuisha angalau wanahabari watano na wawakilishi watano wa asasi za kiraia hukutana kwa lengo la kutathmini hali ya vyombo vya habari katika nchi zao wenyewe. Kwa muda wa siku moja na nusu hivi, jopo hilo hujadili mazingira ya vyombo vya habari kwa kuzingatia vigezo 39 ambavyo hutumika kama adidu za rejea. Mjadala na utoaji wa alama hujadiliwa pamoja mshauri elekezi ambaye pia huhariri taarifa ya AMB. Baada ya kujadili kigezo kimoja, wanajopo huweka alama zao kwenye kigezo husika ambapo huridhiwa kwa kura ya pamoja kwa mujibu wa kielelezo kifuatacho: 2 1 Nchi inakidhi kiashiria 2 Nchi inakidhi vipengele vichache tu vya kiashiria 3 Nchi inakidhi vipengele kadhaa vya kiashiria 4 Nchi inakidhi vipengele vingi vya kiashiria 5 Nchi inakidhi vipengele vyote vya kiashiria KIPIMO CHA VYOMBO VYA HABARI BARANI AFRIKA TANZANIA 2019