ENEO LA 4

4.1 Viwango vya utoaji habari vinafuata kanuni za
msingi za usahihi na haki
Majadiliano yalidhihirisha mgawanyiko mkubwa miongoni mwa washiriki
kuhusu viwango vya utoaji habari katika vyombo vya habari vya Tanzania kwa
kuzingatia haki na usahihi.
Baadhi ya washiriki walikuwa na mtizamo kwamba utoaji wa habari na uchambuzi
kwa ujumla haukuwa wa haki. Matatizo ni pamoja na uwasilishaji hafifu wa
mawazo ya vyanzo vya habari na kuelemea upande wa chama fulani cha siasa
au makundi ya kijamii. Kwa kiasi kikubwa, taarifa za habari na uchambuzi huwa
na tabia ya kufuata mada kuu ya kisiasa na kijamii inayotekelezwa na serikali,
na kutoa nafasi finyu kwa mawazo kinzani. Vyombo vya habari, hususan,
havitaakisi mawazo yanayoikosoa serikali au kutoa mbadala wa misimamo rasmi
iliyotolewa. Mmoja wa washiriki alisema vyombo vya habari vilikuwa na hatia ya
kuendeleza mila potofu, ambazo mara nyingi husababisha mtafaruku miongoni
mwa makabila na dini ndogo.
Kwa upande wa masuala ya kiutamaduni na kiitikadi, kuna tabia ya waandishi
wa habari kuendana na kile kinachoaminiwa na kila mtu. Wakati wa kutoa
habari kuhusu dini fulani, waandishi wa habari hawaendi hatua [moja] mbele
[ili kupata ukweli] na wataegemeza habari zao kwenye kile kinachoaminiwa na
watu wengi zaidi.
Washiriki wengine walisema kwamba mazingira ya kijamii na kisiasa ambayo
waandishi wa habari wanafanyia kazi ni ya kulaumiwa kwa kuwa na upendeleo
katika wigo wa habari. Walisema kwamba, vyombo vya habari vya serikali
vilikuwa na nia yake ya kushadidia msimamo wa serikali na visingeweza
kutarajiwa kujihujumu chenyewe. Walisema kwamba nguvu ya vyombo vya
habari vya serikali na vyanzo vingine vya habari ambavyo viko upande wa serikali
na chama tawala vilivifunika vile vichache vya kujitegemea ambavyo vinatoa
fursa kwa watu wote.
Matatizo ya utoaji habari usio wa haki yalielezewa kuwa na uhusiano wa karibu
na kukosa usahihi. Washiriki walisema kwamba waandishi wa habari mara nyingi
hawakuakisi vichwa vya habari na zinakuwa na majina ambayo yamekosewa
tahajia na taarifa zisizo sahihi. Mshiriki mmoja alisema kwamba ilikuwa kawaida,
mathalan, kwa mwandishi wa habari kutoa maelezo yanayotofautiana kuhusu
tukio moja ambazo hazichagizwi na ukweli bali na itikadi za kisiasa za waandishi.
Kunukuu vibaya vyanzo vya habari, alisema mshiriki, ilikuwa ni kawaida:
Unaweza kuhojiwa na waandishi wawili wa habari. Mmoja atatoa
maelezo sahihi, lakini mwingine atasema kitu kingine tofauti kabisa na
kukihusisha na wewe. Wakati mwingine, maelezo na maoni yanatafsiriwa
isivyo na kupewa mtizamo tofauti kabisa na kile kilichomaanishwa.
Waandishi wa habari walisema viwango duni vinasababishwa na haraka ili
kwenda na muda uliowekwa na kukosekana kwa mifumo imara ya udhibiti

48

KIPIMO CHA VYOMBO VYA HABARI BARANI AFRIKA TANZANIA 2019

Select target paragraph3