ENEO LA 3

3.1 Sheria ya utangazaji inapitishwa na kutekelezwa,
na inatoa mazingira mazuri kwa matangazo ya
umma, biashara na jamii
Washiriki walisema sheria za utangazaji, hasa Sheria ya Mawasiliano ya
Kielektroniki na Posta na Sheria ya Vyombo vya Habari zilikuwa zinabana sana.
Walitolea mfano masharti magumu ya utoaji leseni, ambayo ni pamoja na ada ya
mwaka ya kuongeza muda wa leseni na msururu wa faini, kama vikwazo dhidi
ya ukuaji wa utangazaji kwa watu binafsi na jamii. Pamoja na sifa ya redio za
jamii ya kutotengeneza faida na kujitolea kwa ajili ya maendeleo ya jamii, redio
hizo hazipati upendeleo wowote maalum au msamaha wa kodi.

Alama:
Alama za mshiriki mmoja mmoja:
1

Nchi inakidhi kiashiria

2

Nchi inakidhi vipengele vichache tu vya kiashiria

3

Nchi inakidhi vipengele kadhaa vya kiashiria

4

Nchi inakidhi vipengele vingi vya kiashiria

5

Nchi inakidhi vipengele vyote vya kiashiria

Wastani wa alama:
Alama ya miaka iliyopita:

✓✓
✓✓

✓✓✓✓

✓✓✓

✓

3.3
2006: 2.6; 2008: 2.8; 2010: 2.1; 2012: 3.8; 2015: 3.3

3.2 Utangazaji unadhibitiwa na chombo huru
ambacho kimelindwa ipasavyo dhidi ya kuingiliwa
na sheria, na ambacho bodi yake inateuliwa kwa
uwazi na kushirikisha asasi za kiraia na ambayo
haihodhiwi na chama chochote cha siasa
Utangazaji unadhibitiwa na TCRA. Mamlaka haya yaliyoanzishwa kwa sheria
ya bunge mwaka 2003, yanajinasibu kama‘chombo chenye uhuru-kifani’. Bodi
yake inateuliwa na Rais na waziri mwenye dhamana ya sekta hiyo, kwa kupitia
mchakato wa uteuzi unaoongozwa na katibu mkuu wa wizara husika. Kamati ya
uteuzi inajumuisha wawakilishi wawili wa sekta binafsi lakini haina maamuzi ya
mwisho kuhusu wajumbe wake. Washiriki walisema TCRA haiko huru, pamoja na
kwamba wajumbe wa bodi wanawakilisha wigo mpana wa utaalam. Inawajibika
kwa serikali na kuangalia maslahi ya serikali.

41

KIPIMO CHA VYOMBO VYA HABARI BARANI AFRIKA TANZANIA 2019

Select target paragraph3