ENEO LA 2 2.13 Ukubwa wa soko la utangazaji unawezesha uwepo wa mchanganyiko wa vyanzo vya habari Makampuni ya habari yanalalamika kwamba hawapati matangazo ya biashara ya kutosha ili kuwezesha uendeshaji. Washiriki waliona kwamba, hakika, soko la matangazo ya biashara limedorora kwa miaka mingi na kubakia na watangazaji biashara wachache tu; hasa mashirika ya mawasiliano ya simu, viwanda vya bia na mabenki. Kwenye mijadala, ilionekana kwamba sababu kuu mbili zimebadilisha sura ya soko la matangazo ya biashara Tanzania. Mosi, serikali inadhibiti sehemu kubwa ya matumizi kwenye matangazo ambayo yanarushwa kwa kuvipendelea vyombo vinavyomilikiwa na serikali na vile vya binafsi vyenye kuelemea upande wa serikali. Pili, watoaji wakubwa wa matangazo ya biashara wa zamani sasa wanamiliki vyombo vyao wenyewe vya habari. Hali hii si tu kwamba imebana soko la matangazo ya biashara, lakini pia imeondoa usawa kwenye mgao wa mapato yatokanayo na matangazo ya biashara kwenye tasnia nzima. Mmoja wa washiriki alisema vyombo vya habari pia havikuwa na uwezo wa kuvutia matangazo, akieleza kwamba: Biashara mpya zinaanzishwa kila siku na zinahitaji kutangazwa. Tatizo ni kwamba vyombo vya habari vinawakimbilia watoaji matangazo wale wale. Kama wanatarajia kupata matangazo kutoka serikalini tu na kwenye makampuni machache, basi wanaweza wasipate ya kutosha. Redio za kijamii wanalijua hili na ndo maana wanaenda kwenye sekta isiyo rasmi. Tunatakiwa tuelewe kwamba mambo ni magumu na kuacha kubagua. Ushindani kutoka kwa majukwaa mbadala kama vile mitandao ya kijamii pia umeongezeka. Watu wengi na wafanyabiashara wadogo wameugezia matangazo ya biashara kwenye mtandao. ‘Changamoto kwa vyombo vya habari ni kwenda na mabadiliko haya.’ Alama: Alama za mshiriki mmoja mmoja: 39 1 Nchi inakidhi kiashiria 2 Nchi inakidhi vipengele vichache tu vya kiashiria 3 Nchi inakidhi vipengele kadhaa vya kiashiria 4 Nchi inakidhi vipengele vingi vya kiashiria 5 Nchi inakidhi vipengele vyote vya kiashiria ✓✓ ✓ ✓ ✓ ✓✓✓✓ ✓ ✓ Wastani wa alama: Alama ya miaka iliyopita: 3.0 2006: 2.1; 2008: 1.9; 2010: 2; 2012: 2.5; 2015: 2.2 Jumla ya alama kwenye sekta 2: 2.7 KIPIMO CHA VYOMBO VYA HABARI BARANI AFRIKA TANZANIA 2019 ✓