ENEO LA 2 2.1 Vyombo vingi vya habari (vya kimaandishi, utangazaji, mtandaoni, simu za mkononi) vinapatikana kwa umma na wananchi wanamudu gharama zake Kitakwimu, mandhari ya vyombo vya habari Tanzania ni mchanaganyiko na hai. Mwaka 2018, ilikisiwa kwamba Tanzania Bara ilikuwa na vituo 156 vya redio, vituo 48 vya luninga na magazeti 216, wakati Zanzibar ilikuwa na vituo 25 vya redio, na vituo vya luninga 12.16 Kwa mujibu wa takwimu zilizokusanywa upya na wanajopo, gazeti la Tanzanite ndo lilikuwa la mwisho kusajiliwa mwaka 2015. Vituo vya luninga vya EFM na eTV pia vilianza utangazji mwaka huo huo. Washiriki walisema kwamba vyanzo vya habari vya kawaida vimeweza kukua kwa haraka, hasa katika kipindi cha muongo mmoja uliopita. Hata hivyo, gharama zinazidi kuongezeka na hivyo kupunguza upatikanaji hasa kwa watu maskini waishio vijijini. Mathalan, mabadiliko katika teknolojia ya utangazaji kwa luninga kwa sasa yanailazimu familia ama kununua luninga ya kisasa zaidi au kununua king’amuzi ili kuweza kufaidi chaneli za bure. Kwa bei ya shilingi 1000/= za kitanzania (chini ya nusu ya Dola ya Kimarekani), bei ya gazeti inalingana na ile ya mkate. Kwa mtazamo wa washiriki, inapofikia kuchagua, watu wengi watachagua kununua mkate. Teknolojia ya kidijitali ilipanua wigo wa vyanzo vya habari. Habari kwa njia ya mitandao zimekua kwa kasi zaidi na zinapatikana kwa uraisi zaidi. Pamoja na huduma hizo za kidijitali, magazeti yaliyo mengi, vituo vya redio na luninga vilivyo vingi vinapatikana mtandaoni, na hutumia mitandao ya kijamii kuwafikia watu wengi zaidi. M-Papers, ambao ni mfumo wa habari kidijitali, huwawezesha wananchi kujiunga na huduma za magazeti na majarida kielektroniki. Utafiti wa mandhari ya vyombo vya habari ulihitimisha kwamba ‘Tanzania ilikuwa ikishuhudia mabadiliko ya kimtazamo kwenye anga la kimtandao’.17 Taarifa hiyo iliangazia kwamba: Katika kipindi cha miaka sita iliyopita, matumizi ya mtandao yameongezeka kutoka asilimia 17 mwaka 2012 na kufikia asilima 45 mwaka 2017. Hadi mwezi Septemba 2018, watanzania wapatao 22,995,109 walikuwa na huduma ya mtandao, huku wengi wao (19,006,223) wakitumia mtandao kupitia simu zao za mkononi. Mabadiliko haya, ingawa yanatokea zaidi mijini, yana mchango chanya kwenye upatikanaji wa vyombo vya habari kwa wananchi kwa vile raia wanaweza kufikia vyombo vya habari kupitia mitandao kadha wa kadha ya kijamii. Kwa kuongezea, hali hii inatoa fursa kwa raia kutoa maoni yao kwenye mijadala mbalimbali na ukuaji wa upashaji habari wa kiraia mtandaoni (Spurk&Katunzi, 2018). Upatikanaji wa habari kwa njia ya mtandao unaathiriwa tu na gharama za kupata huduma hiyo. Ingawa watumiaji huhitaji chini ya nusu ya Dola ya Kimarekani 16 Ibid. 17 Ibid. 29 KIPIMO CHA VYOMBO VYA HABARI BARANI AFRIKA TANZANIA 2019