NINI KIFANYIKE 1. Miaka mitatu hadi minne iliyopita, kulikuwa na mabadiliko gani kwenye mazingira ya vyombo vya habari? Mabadiliko Chanya • Kuongezeka kwa idadi ya vyombo vya habari kulikoambatana na kupanuka kwa mitandao ya kijamii kumezuia jaribio la mamlaka kufunga majukwaa ya kujieleza kwa uhuru. • Fursa zaidi za mafunzo yanayojumuisha wadau wapya zimeibuka katika kipindi cha miaka michache iliyopita, na hivyo kuwapa waandishi wa habari wigo mpana zaidi wa kufanya maamuzi. • Vyama vya waandishi wa habari vimekuwa imara zaidi katika kuvilinda vyombo vya habari dhidi ya madhila mbalimbali ya vyombo vya habari na uhuru wa uandishi wa habari. Mabadiliko Hasi 2. 61 • Fursa za kisiasa na vyombo vya habari zinasinyaa, hasa kutokana na kuanzishwa kwa sheria kandamizi tangu mwaka 2015. • Ongezeko la matumizi ya wataalam wapotoshaji kwenye mitandao ya kijamii ili kudhibiti uhuru wa kujieleza kumesababisha athari mbaya, na hivyo kuzuia uhuru wa kujieleza. • Wanawake wamezidi kuwa na taswira hasi mbele ya viongozi waandamizi wa serikali na kwenye vyombo vya habari. • Imekuwa ni vigumu sana kupata vyanzo vya habari, hususan kutoka kwenye ofisi za umma. Ni jitihada gani zinahitajika katika kipindi cha miaka mitatu hadi minne ijayo? • Kuna haja ya kuwa na mikakati ya kisheria na ushawishi dhidi ya sheria kandamizi, na harakati hizi zinaweza kuongozwa na CORI. • Kuna haja ya kuongeza mafunzo kuhusu usalama wa vyombo vya habari na mchanganyiko, na harakati hizi zinaweza kuongozwa na UNESCO/TMF/ MCT/THRDC. • Kuna haja ya kundelea kufanya ushawishi kwa ajili ya kufufua vyama vya wafanyakazi wa vyombo vya habari na kuungana na Shirikisho la Kimataifa la Waandishi wa Habari. • Kuna haja ya makampuni ya vyombo vya habari kufanya jitihada za maksudi kwa minajili ya kurasimisha mafunzo na kutengeneza fursa zaidi za mafunzo kwenye maudhui yanayowalenga watu wenye ulemavu, jinsia na haki za binadamu. KIPIMO CHA VYOMBO VYA HABARI BARANI AFRIKA TANZANIA 2019